UHURU FM
Wakulima wa miwa waanza kunufaika.

UAMUZI wa Rais John Magufuli kusimiamia bei ya Sukari na kuzuia Sukari kutoka nje ya nchi kuingizwa nchini, umekiwezesha Kiwanda cha Sukari Kilombero, kulipa Wakulima bei ya juu ambayo haijawahi kulipwa katika Historia ya Wakulima na Kiwanda hicho tangu kianzishwe.

Kauli hiyo imetolewa na Kiongozi wa Timu ya Wakulima wa Nje, JOB ZAHORO na kuthibitishwa na wakulima wenyewe wakati wa Siku ya Wakulima iliyoandaliwa na Watafiti kutoka Taasisi ya utafiti wa Miwa Kibaha, mara baada ya kutembelea Mashamba Darasa ya Miwa huko Kilombero Mkoani Morogoro.

Hivi sasa Kiwanda cha Sukari cha Kilombero kinawalipa Wakulia zaidi ya shilingi laki moja kwa tani ya Miwa kwa msimu ulioisha kutoka kiasi cha shilingi Elfu-79, ya msimu uliopita.

Kumekuwa na ongezeko la malipo kwa ujumla kwa Wakulima wa nje tangu kiwanda hicho kuanzishwa mwaka 1999.            

RECENTS
MICHEZO
KOCHA wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars Salum Mayanga ameita kikosi cha wacheza 24 watakaoingia kambini kwa ajili ya mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Benin.
October 24, 2017
Read More
Mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya Young Africans na Simba utafanyika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam kama ilivyotangazwa awali. Hakuna mabadiliko.
October 23, 2017
Read More
HABARI ZA JUU
KITAIFA
BUNGE limepitisha marekebisho ya sheria ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya wa mwaka 2017 yenye lengo la kuboresha utekelezaji wa sheria na kuondoa upungufu uliojitokeza wakati wa kuitumia sheria hiyo.
November 17, 2017
Read More
MAAFISA kutoka Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Abeid Amani Karume cha Zanzibar (AAKIA), wamefurahishwa na namna ulinzi na usalama wa abiria na mali zao unavyofanywa kwenye Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), imeelezwa.
November 15, 2017
Read More
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan leo amefungua mkutano wa pili wa Biashara, Ujasiriamali na Maonyesho wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ulioandaliwa na Baraza la Biashara la Afrika Mashariki.
November 14, 2017
Read More
KATIKA kuhakikisha Vijana wengi zaidi wanapata Elimu ya Ufundi, Serikali inaendelea na Mpango wake wa Ujenzi wa Vyuo vya Ufundi 43 katika Wilaya mbalimbali nchini.
November 14, 2017
Read More