UHURU FM
Kampuni ya FlyDubai yatangaza kuanza safari za Dubai/Kilimanjaro.

KAMPUNI ya Usafiri wa Ndege ya Flydubai yenye Ofisi zake Kuu Dubai imetangaza mwanzo wa Safari za Ndege zake toka Dubai hadi Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro, Tanzania kuanzia Oktoba 29 mwaka huu.

Huduma ya usafiri inamaanisha kuwa Kampuni hiyo, licha ya kuwasafirisha wateja hadi Dar es Salaam na Zanzibar, sasa itakuwa na Vituo 12 kwa jumla Barani Afrika.

Kampuni ya Flydubai ilianzisha operesheni zake nchini Tanzania Mwaka 2014 na imepata ongezeko kuu la wasafiri kwa miaka michache iliyopita.

Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro utapata Safari Sita kwa wiki na Tatu miongoni mwake zitakuwa kupitia kwa Jiji Kuu la Dar es Salaam.

Afisa Mkuu Mtendaji wa Kampuni ya Flydubai, GHAITH AL GHAITH, amesema Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro upo kati ya maeneo ya Kilimanjaro na Arusha Kaskazini mwa Tanzania.

Uwanja huo ndio kiingilio cha eneo la Kilimanjaro ambalo linajumlisha maeneo ya Mlima Kilimanjaro, Hifadhi ya Wanyama-Pori ya Arusha, Ngorongoro Crater na Hifadhi ya Wanyama-Pori ya Serengeti.

RECENTS
MICHEZO
KIKOSI kamili cha wachezaji 25 wa klabu ya Everton kimetua rasmi asubuhi hii jijini Dar es Salaam tayari kwa ajili ya mchezo wao wa kirafiki dhidi ya timu ya Gor Mahia ya Kenya.
July 12, 2017
Read More
WAZIRI wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe, amesitisha uteuzi wa Mwenyekiti na Wajumbe wote wa Baraza la Michezo la Taifa kuanzia leo Julai 10 2017 kufuatia Baraza hilo kushindwa kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya Michezo.
July 10, 2017
Read More
HABARI ZA JUU
KITAIFA
July 21, 2017
Read More
July 21, 2017
Read More
July 21, 2017
Read More
July 21, 2017
Read More