UHURU FM
Everton watua nchini tayari kuikabili Gor Mahia.

KIKOSI kamili cha wachezaji 25 wa klabu ya Everton kimetua rasmi asubuhi hii jijini Dar es Salaam tayari kwa ajili ya mchezo wao wa kirafiki dhidi ya timu ya Gor Mahia ya Kenya.

Ziara hiyo ya Everton iliyoratibiwa na wadhamini wao kampuni ya michezo ya kubahatisha ya Sportpesa yenye makao yake nchini Kenya, ni sehemu ya maandalizi ya timu hiyo kwa ajili ya msimu mpya wa Ligi Kuu nchini Uingereza.

Mara baada ya kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, kikosi hicho cha Everton kililakiwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe.

Miongozi mwa wachezaji waliosafiri na kikosi hicho ni pamoja na mshambuliaji wa zamani wa Manchester United Wayne Rooney ambaye amesajili kipindi hiki cha majira ya kiangazi na klabu hiyo.

Everton anatarajiwa kucheza na Gor Mahia kesho katika Uwanja wa Taifa, mchezo ambao utaanza majira ya saa 11 za jioni.

RECENTS
MICHEZO
KIKOSI kamili cha wachezaji 25 wa klabu ya Everton kimetua rasmi asubuhi hii jijini Dar es Salaam tayari kwa ajili ya mchezo wao wa kirafiki dhidi ya timu ya Gor Mahia ya Kenya.
July 12, 2017
Read More
WAZIRI wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe, amesitisha uteuzi wa Mwenyekiti na Wajumbe wote wa Baraza la Michezo la Taifa kuanzia leo Julai 10 2017 kufuatia Baraza hilo kushindwa kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya Michezo.
July 10, 2017
Read More
HABARI ZA JUU
KITAIFA
July 21, 2017
Read More
July 21, 2017
Read More
July 21, 2017
Read More
July 21, 2017
Read More