UHURU FM
Mjane wa Rais Mandela alia na mimba za utotoni nchini Tanzania

SERIKALI imetakiwa kuongeza juhudi katika kukabiliana na wimbi la ongezeko la Ndoa na Mimba za Utotoni linalokatisha ndoto za wasichana kielimu.         

Wito huo umetolewa na Mwanaharakati maarufu wa haki za binadamu Barani Afrika, GRACA MACHEL, wakati wa ziara maalumu ya kukagua miradi ya afya katika kijiji cha Mpamantwa Wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma.

MACHEL ambaye ni Mjane wa Mke wa Rais wa zamani wa Afrika ya Kusini, NELSON MANDELA, amesema inasikitisha kuona namna ambavyo maisha ya wasichana wadogo yanakatishwa na baadhi ya watu wazima wasiokuwa na hofu ya Mungu ndani yao.

Tanzania ni miongoni mwa nchi Barani Afrika zinazokabiliana na changamoto kubwa ya Ndoa za Utotoni ambazo kwa kiasi kikubwa zinawanyima wasichana haki zao za msingi za kikatiba na kibinadamu.

Licha ya kupongeza uamuzi wa serikali kuhusu wanafunzi wanaopata Mimba kutoruhusiwa kurudi Shuleni, GRACA MACHEL, amesema jitihada za serikali chini ya Rais JOHN MAGUFULI ya kutoa elimu bure haitazaa matunda iwapo suala la Mimba za Utotoni halitakomeshwa.

RECENTS
MICHEZO
KIKOSI kamili cha wachezaji 25 wa klabu ya Everton kimetua rasmi asubuhi hii jijini Dar es Salaam tayari kwa ajili ya mchezo wao wa kirafiki dhidi ya timu ya Gor Mahia ya Kenya.
July 12, 2017
Read More
WAZIRI wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe, amesitisha uteuzi wa Mwenyekiti na Wajumbe wote wa Baraza la Michezo la Taifa kuanzia leo Julai 10 2017 kufuatia Baraza hilo kushindwa kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya Michezo.
July 10, 2017
Read More
HABARI ZA JUU
KITAIFA
July 21, 2017
Read More
July 21, 2017
Read More
July 21, 2017
Read More
July 21, 2017
Read More