UHURU FM
TAA yatakiwa kutokuwa tegemezi

MAMLAKA ya Viwanja vya Ndege Tanzania-TAA, imetakiwa kuhakikisha kuwa Viwanja vya Ndege vilivyoboreshwa vinajisimamia na kujiendesha vyenyewe ili viache kutegemea Mapato kutoka Kiwanja cha Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere kwa ajili ya shughuli zao za kila siku.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa MAKAME MBARAWA, ametoa agizo hilo baada ya kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa kiwanja cha ndege cha tabora ambapo mpaka sasa umefikia Asilimia 96 na umegharimu shilingi Bilioni-27.

Hata hivyo, Profesa MBARAWA, amesisitiza kuwa gharama za usafiri wa Anga zitaendelea kupungua kadri huduma na ubora zitavyokuwa zinaendelea kuongezeka ili kuwezesha Abiria wengi kutumia usafiri huo na hivyo kuwezesha pato la Taifa kuongezeka.

Kwa upande wake, Meneja wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Mkoa wa Tabora, DANSTAN KOMBA, amesema idadi ya abiria wanaotumia Kiwanja cha Ndege hicho imeongezeka kutoka Asilimia 10 kwa mwaka 2011 hadi kufikia Asilimia 62.3 mwaka 2016, baada ya Ndege za ATCL kuanza safari zake Mkoani Tabora.

RECENTS
MICHEZO
KIKOSI kamili cha wachezaji 25 wa klabu ya Everton kimetua rasmi asubuhi hii jijini Dar es Salaam tayari kwa ajili ya mchezo wao wa kirafiki dhidi ya timu ya Gor Mahia ya Kenya.
July 12, 2017
Read More
WAZIRI wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe, amesitisha uteuzi wa Mwenyekiti na Wajumbe wote wa Baraza la Michezo la Taifa kuanzia leo Julai 10 2017 kufuatia Baraza hilo kushindwa kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya Michezo.
July 10, 2017
Read More
HABARI ZA JUU
KITAIFA
July 21, 2017
Read More
July 21, 2017
Read More
July 21, 2017
Read More
July 21, 2017
Read More