UHURU FM
Kiwanda cha ngozi suluhisho la tatizo la ajira Moshi

MAWAZIRI  Watatu wameelezea kufurahishwa na maendeleo ya ujenzi na uboreshaji wa Kiwanda cha bidhaa za Ngozi cha Karanga kinachomilikiwa na Jeshi la Magereza nchini, kilichopo Mkoani Kilimanjaro.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu, JENISTA MHAGAMA, amesema Kiwanda hicho pekee kitatoa ajira za moja kwa moja 689 na zisizo za moja kwa moja 1,800, hivyo kusaidia kukabiliana na changamoto ya ajira hasa kwa vijana nchini.

Naye, Waziri wa Fedha na Mipango, Dokta PHILIP MPANGO, ametaka kuharakishwa ujenzi wa kiwanda hicho cha Ngozi ili uzalishaji uanze na hatimaye nchi inufaike.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, HAMAD MASAUNI, ameishauri Mifuko mingine ya Pesheni kutumia fursa zilizopo Jeshi la Magereza ikiwamo maeneo na rasilimali watu kufikia azama ya serikali ya kuwa na Uchumi wa kati kupitia Viwanda.

Kiwanda hicho kinachojengwa kwa ushirikiano na Mfuko wa Pensheni wa PPF, kitagharimu zaidi ya shilingi Bilioni-54 na kitakuwa pia na uwezo wa kuzalisha Futi Mraba za Ngozi Milioni Tatu, Laki Saba na Nusu kwa mwaka.

RECENTS
MICHEZO
KIKOSI kamili cha wachezaji 25 wa klabu ya Everton kimetua rasmi asubuhi hii jijini Dar es Salaam tayari kwa ajili ya mchezo wao wa kirafiki dhidi ya timu ya Gor Mahia ya Kenya.
July 12, 2017
Read More
WAZIRI wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe, amesitisha uteuzi wa Mwenyekiti na Wajumbe wote wa Baraza la Michezo la Taifa kuanzia leo Julai 10 2017 kufuatia Baraza hilo kushindwa kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya Michezo.
July 10, 2017
Read More
HABARI ZA JUU
KITAIFA
July 21, 2017
Read More
July 21, 2017
Read More
July 21, 2017
Read More
July 21, 2017
Read More