UHURU FM
Katibu wa Chadema Arusha ajiuzulu

KATIBU wa Chama Cha Democrasia na Maendeleo Mkoa wa Arusha, ambaye pia ni Meya wa Jiji la Arusha, CALIST LAZARO, ametangaza kujiuzulu nafasi ya Katibu wa Chama hicho, akisema amekuwa na majukumu mengi, hivyo ameamua kuachia ngazi nafasi hiyo.

Habari ambazo ni za uhakika zilizoifikia Uhuru FM, zinasema Meya huyo wa Arusha tayari ameandika barua ya kujiuzulu, akidai kuwa amekuwa na majukumu mengi hivyo hawezi tena kuendelea kutumikia nafasi ya Ukatibu wa Mkoa wa Chama hicho.

Katika siku za hivi karibuni Madiwani Sita kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha wametangaza kujiuzulu Udiwani na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi wakisema wamevutiwa na utendaji kazi wa Rais JOHN MAGUFULI.

Wachambuzi wa Masuala ya Siasa nchini, wanasema kama hali hiyo inayoendelea katika Mikoa ya Kanda ya Kaskazini itaendelea, basi huenda hadi kufikia mwaka 2020, Chama Cha Chadema kinaweza kupotea kabisa katika medali ya Siasa.

RECENTS
MICHEZO
KIKOSI kamili cha wachezaji 25 wa klabu ya Everton kimetua rasmi asubuhi hii jijini Dar es Salaam tayari kwa ajili ya mchezo wao wa kirafiki dhidi ya timu ya Gor Mahia ya Kenya.
July 12, 2017
Read More
WAZIRI wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe, amesitisha uteuzi wa Mwenyekiti na Wajumbe wote wa Baraza la Michezo la Taifa kuanzia leo Julai 10 2017 kufuatia Baraza hilo kushindwa kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya Michezo.
July 10, 2017
Read More
HABARI ZA JUU
KITAIFA
July 21, 2017
Read More
July 21, 2017
Read More
July 21, 2017
Read More
July 21, 2017
Read More