UHURU FM
Wananchi waomba waongezewe muda wa kulipa kodi za majengo

WAKATI leo ikiwa ndio siku ya mwisho wa muda wa nyongeza wa wiki mbili uliowekwa na Mamlaka ya Mapato Nchini-TRA, kwa wananchi kulipia Kodi ya Majengo bila adhabu, baadhi ya wananchi wameiomba Serikali kuongeza muda mwingine zaidi ili kutoa fursa kwa wananchi wengi kulipia.

Wamedai kuwa kumekuwa na changamoto ya idadi ndogo ya watumishi wa TRA hatua inayosababisha kuwepo kwa misururu mirefu ya wananchi wanaofika katika Ofisi za TRA kulipia Kodi ya Majengo, hivyo hali hiyo imekuwa ikichangia wananchi wengi kushindwa kulipa.

Wamesema mwamko wa wananchi kulipa kodi ni mkubwa licha ya uwepo wa foleni kubwa kila mahali nchini kutokana na upungufu wa watumishi wa TRA pamoja na vitendea kazi kama vile Kompyuta na Mashine za Kielektroniki za kutolea Risiti-EFDs.

 Waziri wa Fedha na Mipango, Dokta PHILIP MPANGO, amewaomba wananchi kuwa watulivu, huku akiahidi kutatua changamoto ya upungufu wa watumishi na vitendea kazi ili kuwaondolea kero wananchi waliojitokeza kwa Moyo kulipa kodi mbalimbali ikiwemo ya Majengo.

RECENTS
MICHEZO
KIKOSI kamili cha wachezaji 25 wa klabu ya Everton kimetua rasmi asubuhi hii jijini Dar es Salaam tayari kwa ajili ya mchezo wao wa kirafiki dhidi ya timu ya Gor Mahia ya Kenya.
July 12, 2017
Read More
WAZIRI wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe, amesitisha uteuzi wa Mwenyekiti na Wajumbe wote wa Baraza la Michezo la Taifa kuanzia leo Julai 10 2017 kufuatia Baraza hilo kushindwa kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya Michezo.
July 10, 2017
Read More
HABARI ZA JUU
KITAIFA
July 21, 2017
Read More
July 21, 2017
Read More
July 21, 2017
Read More
July 21, 2017
Read More