UHURU FM
Tanzania, Kenya kuunda kamati kutatua migogoro ya kibiashara

Tanzania na Kenya zimekubaliana kwa pamoja pendekezo la kuunda Kamati ndogo itakayokuwa na jukumu la kutafuta suluhu ya haraka inapotokea migogoro ya Kibiashara kati ya nchi hizo Mbili.

Makubalianao hayo yamefikiwa baada ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya, AMINA MOHAMMED kuwasilisha Ujumbe Maalum kutoka kwa Rais wa Kenya, UHURU KENYATA kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dokta AUGUSTINE MAHIGA.

Ujumbe huo kutoka kwa Rais KENYATTA unakuja kwa Rais JOHN MAGUFULI ambapo umepokewa na Waziri MAHIGA jijini Dar es Salaam kwa niaba ya Rais.

Kamati hiyo itaongozwa na wao wenyewe ambayo itakuwa na jukumu la kutafuta suluhu ya haraka inapotokea migogoro ya kibiashara kati ya nchi hizo mbili.

RECENTS
MICHEZO
KOCHA wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars Salum Mayanga ameita kikosi cha wacheza 24 watakaoingia kambini kwa ajili ya mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Benin.
October 24, 2017
Read More
Mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya Young Africans na Simba utafanyika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam kama ilivyotangazwa awali. Hakuna mabadiliko.
October 23, 2017
Read More
HABARI ZA JUU
KITAIFA
BUNGE limepitisha marekebisho ya sheria ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya wa mwaka 2017 yenye lengo la kuboresha utekelezaji wa sheria na kuondoa upungufu uliojitokeza wakati wa kuitumia sheria hiyo.
November 17, 2017
Read More
MAAFISA kutoka Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Abeid Amani Karume cha Zanzibar (AAKIA), wamefurahishwa na namna ulinzi na usalama wa abiria na mali zao unavyofanywa kwenye Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), imeelezwa.
November 15, 2017
Read More
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan leo amefungua mkutano wa pili wa Biashara, Ujasiriamali na Maonyesho wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ulioandaliwa na Baraza la Biashara la Afrika Mashariki.
November 14, 2017
Read More
KATIKA kuhakikisha Vijana wengi zaidi wanapata Elimu ya Ufundi, Serikali inaendelea na Mpango wake wa Ujenzi wa Vyuo vya Ufundi 43 katika Wilaya mbalimbali nchini.
November 14, 2017
Read More