UHURU FM
Waumini wafa maji wakiwa katika ibada ya ubatizo rombo

Waumini wawili wa dhehebu la Pentekoste kutoka kanisa la Solohamu lililopo eneo la Keni Kituo cha Afya wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro, wamefariki dunia kufuatia kuzama kwenye maji ya kina kirefu katika mto Ungwasi unaotenganisha Tarafa za Mkuu na Mashati wilayani humo.

Tukio hilo limetokea jana Jumapili majira ya saa 8 mchana ambapo waumini wa dhehebu hilo walikuwa kwenye ratiba ya ibada ya ubatizo ambayo iliambatana na maombi yaliyokuwa yakifanyika sambamba na ibada hiyo iliyoisha vibaya kwa kuondoka na roho za waumini wawili wanaokadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 30 hadi 35.

Diwani wa Kata ya Mraokeryo ambayo iko mpakani mwa mto Ungwasi Mh. Athumani Kimario amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo anaeleza kuwa waumini hao wamezama kwenye dimbwi la mto Ungwasi eneo liitwalo Kwalani karibu kabisa na daraja kuu la Ungwasi.

"Ni kweli,nilipata taarifa kutoka kwa bwana mmoja anaitwa Abraham Canal ambaye naye amepata taarifa kwa muumini ambaye ni boda boda, na amemueleza kwamba kuna mabwana wawili wamezama hapo Kwalani wakiwa kwenye ibada ya ubatizo", Amesema diwani huyo. 


Taarifa za awali zinaeleza kuwa mmoja wa waumini alipatwa na mapepo akiwa kwenye ibada na akawa anaingia kwenye maji hali ambayo ilipelekea mwenzake kumkimbilia ili kujaribu kumuokoa lakini juhudi zake hazikuzaa matunda kwani wote walitumbukia kwenye maji hayo yenye kina kirefu na kufariki dunia baada ya muda mfupi kufuatia kukosa pumzi wakiwa kwenye maji hayo. 


Aidha, Jeshi la polisi tayari limeichukua miili hiyo iliyoopolewa na vijana wa bodaboda wakishirikiana na wakazi wa eneo hilo na tayari miili hiyo imesafirishwa na imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya Huruma wilayani humo.

Dhehebu la pentekoste ni mojawapo ya madhehebu ambayo ubatizo wake huusisha maji ya kina kirefu ambapo waumini wanaobatizwa huzamishwa kwa sekunde kadhaa ikiwa ni ishara ya kukifuata kile ambacho alifanyiwa Yesu Kristo katika mto Yordani.

RECENTS
MICHEZO
KIKOSI kamili cha wachezaji 25 wa klabu ya Everton kimetua rasmi asubuhi hii jijini Dar es Salaam tayari kwa ajili ya mchezo wao wa kirafiki dhidi ya timu ya Gor Mahia ya Kenya.
July 12, 2017
Read More
WAZIRI wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe, amesitisha uteuzi wa Mwenyekiti na Wajumbe wote wa Baraza la Michezo la Taifa kuanzia leo Julai 10 2017 kufuatia Baraza hilo kushindwa kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya Michezo.
July 10, 2017
Read More
HABARI ZA JUU
KITAIFA
July 21, 2017
Read More
July 21, 2017
Read More
July 21, 2017
Read More
July 21, 2017
Read More