UHURU FM
TANROADS imelazimika kupunguza kona za barabara Tanga

WAKALA wa Barabara Nchini-TANROADS, Mkoa wa Tanga, umelazimika kupunguza kona za barabara ya kuelekea Kata ya Chongoleani ili kurahisisha msafara wa Marais JOHN MAGUFULI na YOWERI MUSEVENI wa Uganda, watakaowasili hivi karibuni kuzindua mradi wa ujenzi wa Bomba la Mafuta.

Meneja wa Tanroads Mkoa wa Tanga, ALFRED NDUMBARO ametoa taarifa hiyo leo wakati akizuinguimza na Mwananchi kuhusu maandalizi ya uzinduzi wa mradi wa Bomba la Mafuta lenye urefu wa Kilomita 1,403 kutoka Hoima, Uganda hadi Tanga.

Marais hao Wawili wa Tanzania na Uganda wanatarajiwa kufika Chongoleani mwishoni mwa mwezi huu au mwanzoni mwa Agosti.

NDUMBARO amesema Tanroads imelazimika kupunguza kona za barabara hiyo ambayo ilikuwa na urefu wa kilomita Nane na sasa imefikia Kilomita Saba ili kurahisisha Magari yatakayokuwa kwenye msafara wa Marais hao.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, MARTINE SHIGELA, amesema maandalizi ya kuwapokea Marais hao kwa ajili ya uzinduzi wa mradi huo yameshakamilika.

 

RECENTS
MICHEZO
KIKOSI kamili cha wachezaji 25 wa klabu ya Everton kimetua rasmi asubuhi hii jijini Dar es Salaam tayari kwa ajili ya mchezo wao wa kirafiki dhidi ya timu ya Gor Mahia ya Kenya.
July 12, 2017
Read More
WAZIRI wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe, amesitisha uteuzi wa Mwenyekiti na Wajumbe wote wa Baraza la Michezo la Taifa kuanzia leo Julai 10 2017 kufuatia Baraza hilo kushindwa kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya Michezo.
July 10, 2017
Read More
HABARI ZA JUU
KITAIFA
July 21, 2017
Read More
July 21, 2017
Read More
July 21, 2017
Read More
July 21, 2017
Read More