UHURU FM
TBA yapewa miezi 6 kukamilisha ujenzi wa nyumba ya Jaji Shinyanga

WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, ameutaka Wakala wa Majengo Tanzania-TBA, kuhakikisha ndani ya miezi Sita wanakamilisha ujenzi wa Nyumba ya Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Shinyanga.

Profesa Mbarawa ametoa agizo hilo wakati akikagua miradi mbalimbali inayotekelezwa na TBA ambapo pamoja na mambo mengine amesisitiza umuhimu wa kuwapatia Majaji mahali pazuri pa kuishi ili watimize wajibu wao wa kutenda haki kwa wananchi ipasavyo.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Shinyanga Jaji Richard Kibella, amemshukuru Profesa Mbarawa kwa niaba ya taasisi zake za TBA na Wakala wa Ufundi na Umeme-TEMESA kwa namna ambavyo wameshirikiana na Mahakama kukamilisha ujenzi wa Jengo hilo na kuwapatia huduma nyingine za uendeshaji.

Ameiomba Serikali kukamilisha haraka ujenzi wa Nyumba za viongozi na watumishi wa Mahakama kwani gharama kubwa zinatumika katika malipo ya Pango.

 

RECENTS
MICHEZO
KIKOSI kamili cha wachezaji 25 wa klabu ya Everton kimetua rasmi asubuhi hii jijini Dar es Salaam tayari kwa ajili ya mchezo wao wa kirafiki dhidi ya timu ya Gor Mahia ya Kenya.
July 12, 2017
Read More
WAZIRI wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe, amesitisha uteuzi wa Mwenyekiti na Wajumbe wote wa Baraza la Michezo la Taifa kuanzia leo Julai 10 2017 kufuatia Baraza hilo kushindwa kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya Michezo.
July 10, 2017
Read More
HABARI ZA JUU
KITAIFA
July 21, 2017
Read More
July 21, 2017
Read More
July 21, 2017
Read More
July 21, 2017
Read More