UHURU FM
Dokta Kijazi awapa somo Watanzanaia

Watanzania wametakiwa kujiwekea utaratibu wa kuangalia Afya zao mara kwa mara ili kuhakikisha wakati wote Afya zinakuwa Salama.

Wito huo umetolewa leo na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi JOHN KIJAZI akiwa ni mmoja wa waombolezaji waliofika kwenye Msiba wa Mke wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dokta HARRISON MWAKYEMBE, LINAH MWAKYEMBE aliyefariki Dunia juzi Usiku kutokana na ugonjwa wa Saratani ya Titi.

Pia Balozi KIJAZI, ambaye ni miongoni mwa viongozi waliofika Nyumbani kwa Waziri Mwakyembe, kuomboleza kifo cha Mkewe, amewaomba Watanzania kuwa na utamaduni wa kufanya Mazoezi ili kujiweka mbali na magonjwa yasiyoambukiza.

Wakati huo huo, Mwili wa Marehemu LINAH MWAKYEMBE, unatarajiwa kuagwa kesho kuanzia Asubuhi, Kunduchi Beach na kisha baadaye Majira ya Mchana utasafirishwa kwa Ndege kwenda Wilayani Kyela Mkoani Mbeya kwa ajili ya maziko yaliyopangwa kufanyika keshokutwa.

RECENTS
MICHEZO
KIKOSI kamili cha wachezaji 25 wa klabu ya Everton kimetua rasmi asubuhi hii jijini Dar es Salaam tayari kwa ajili ya mchezo wao wa kirafiki dhidi ya timu ya Gor Mahia ya Kenya.
July 12, 2017
Read More
WAZIRI wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe, amesitisha uteuzi wa Mwenyekiti na Wajumbe wote wa Baraza la Michezo la Taifa kuanzia leo Julai 10 2017 kufuatia Baraza hilo kushindwa kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya Michezo.
July 10, 2017
Read More
HABARI ZA JUU
KITAIFA
July 21, 2017
Read More
July 21, 2017
Read More
July 21, 2017
Read More
July 21, 2017
Read More