UHURU FM
hakuna mchele wa plastiki nchini - Serikali.

SERIKALI kupitia Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, imewahakikishia Watanzania huku ikisema hakuna Mchele wa Plastiki nchini, na kinachofanyika sasa ni Siasa ambazo zinafanywa na baadhi ya watu ili kudhoofisha mauzo ya Mchele wa Tanzania nje ya nchi.

Waziri wa Wizara hiyo, CHARLES MWIJAGE, ameiambia uhuru fm kuwa hakuna mchele huo unaodaiwa kuingiza hapa nchini na kwamba serikali kupitia mamlaka zake imefanya uchunguzi na kubaini kuwa hakuna ukweli kuhusu madai hayo ya mchele wa plastiki.

Wakati huo huo, Waziri MWIJAGE ametangaza mpango utakaowahusu Wafanyabiashara wakubwa na Wajasiriamali ambapo kuanzia sasa atakuwa anasafiri nao nje ya nchi ili kuwajengea uwezo kujitangaza na kutangaza bidhaa wanazozalisha hapa nchini ili kupata Masoko nje ya nchi.

Safari ya kwanza Wafanyabiashara wakubwa na Wajasiriamali itakuwa Julai 29 mwaka huu na watakwenda nchini Vetinam ambapo watajilipia nauli na malazi.

RECENTS
MICHEZO
KUTAKUWA na mtihani na zoezi la utimamu wa mwili (Fitness Test) kwa ajili ya waamuzi wa madaraja ya Tatu na Pili ili kuweza kuwapandisha madaraja kwa mujibu wa utaratibu.
October 09, 2017
Read More
RWANDA na Sudani zimethibitisha kushiriki katika mashindano ya kuogelea ya kanda ya tatu ya Afrika (Cana zone 3) yaliyopangwa kufanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba 19 -21.
September 26, 2017
Read More
HABARI ZA JUU
KITAIFA
SERIKALI haitaweza kuwavumilia watendaji wazembe katika suala zima la uvamizi wa mifugo hususan ng’ombe kutoka katika nchi jirani ya Kenya.
October 16, 2017
Read More
NAIBU Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa ameishauri Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Kilimo ukanda wa Kitropiki (IITA) kuongeza kasi ya utoaji elimu kwa wakulima nchini kuhusu kadhia ya Sumu Kuvu.
October 16, 2017
Read More
WANACHAMA wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) 113 kutoka bara na visiwani wamejitokeza kuwania nafasi ya uenyekiti Taifa katika uchaguzi utakaofanyika mwaka huu, idadi ambayo haijawahi kutokea tangu kuanzishwa kwa umoja huo.
October 16, 2017
Read More
HATIMAYE Katibu Mkuu wa Baraza la Mashirika ya Kiislamu Nchini, Sheikh ISSA PONDA, leo amejisalimisha katika Kituo cha Polisi cha Central, kufuatia agizo la Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam, LAZARO MAMBOSASA.
October 13, 2017
Read More