UHURU FM
Tanzania,Uganda zatiliana saini Mkataba wa uzalishaji Umeme

Serikali za Tanzania na Uganda zimetiliana saini Mkataba wa Makubaliano ya Awali wa kupeleka Umeme kwenye Vijiji vya Mpakani mwa nchi hizo.

Hati ya Makubaliano hayo imesainiwa Mjini Bukoba, Mkoani Kagera na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi AUGUSTINE MAHIGA akiwakilisha Wizara ya Nishati na Madini wa Tanzania na Waziri wa Nishati wa Uganda, Dokta SIMON D’UJANGA.

Makubaliano ya msingi katika Hati iliyosainiwa ni utekelezaji wa Mradi wa kupeleka umeme kwenye vijiji vya Nangoma, katika eneo lililopo Mpakani mwa Tanzania na Uganda na Vijiji vingine vya maeneo hayo kwa kutokea upande wa Tanzania.

Akifafanua kuhusu makubaliano hayo, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dokta MEDARD KALEMANI, amesema Wakala wa Nishati Vijijini kwa upande wa Tanzania, utahusika katika kugharamia ujenzi wa njia ya umeme ya msongo wa Kilovoti 33 kufikisha umeme katika eneo la Mpakani, umbali wa Kilomita 0.8.

RECENTS
MICHEZO
KUTAKUWA na mtihani na zoezi la utimamu wa mwili (Fitness Test) kwa ajili ya waamuzi wa madaraja ya Tatu na Pili ili kuweza kuwapandisha madaraja kwa mujibu wa utaratibu.
October 09, 2017
Read More
RWANDA na Sudani zimethibitisha kushiriki katika mashindano ya kuogelea ya kanda ya tatu ya Afrika (Cana zone 3) yaliyopangwa kufanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba 19 -21.
September 26, 2017
Read More
HABARI ZA JUU
KITAIFA
SERIKALI haitaweza kuwavumilia watendaji wazembe katika suala zima la uvamizi wa mifugo hususan ng’ombe kutoka katika nchi jirani ya Kenya.
October 16, 2017
Read More
NAIBU Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa ameishauri Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Kilimo ukanda wa Kitropiki (IITA) kuongeza kasi ya utoaji elimu kwa wakulima nchini kuhusu kadhia ya Sumu Kuvu.
October 16, 2017
Read More
WANACHAMA wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) 113 kutoka bara na visiwani wamejitokeza kuwania nafasi ya uenyekiti Taifa katika uchaguzi utakaofanyika mwaka huu, idadi ambayo haijawahi kutokea tangu kuanzishwa kwa umoja huo.
October 16, 2017
Read More
HATIMAYE Katibu Mkuu wa Baraza la Mashirika ya Kiislamu Nchini, Sheikh ISSA PONDA, leo amejisalimisha katika Kituo cha Polisi cha Central, kufuatia agizo la Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam, LAZARO MAMBOSASA.
October 13, 2017
Read More