UHURU FM
Waziri Mkuu akagua miradi wilaya ya Mbeya Mjini.

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa, ametembelea Kiwanda cha Kampuni ya SBC-Tanzania Ltd pamoja na Kiwanda cha Kiwanda cha Kukata na Kung’arisha Mawe ya Asili cha Marmo Granito Mines Tanzania Ltd, vilivyoko Iyunga Mjini Mbeya, na kuwataka Watanzania kupenda kununua bidhaa za ndani.

Amevitembelea Viwanda hivyo ili kukagua utekelezaji wa sera ya kujenga Uchumi wa Viwanda nchini, ambao ndiyo kipaumbe cha Serikali ya Awamu ya Tano.

Akiwa katika Kiwanda cha Pepsi kilichojengwa mwaka 1999 kikiwa na Wafanyakazi 75 na hivi sasa kina Wafanyakazi 190, amewataka Watanzania kupenda kutumia bidhaa zinazozalishwa kwenye Viwanda vya ndani.

Akiwa katika Kiwanda cha Marmo Granito Mines Tanzania Ltd, Waziri Mkuu, amesema mbali na kukuza uchumi na kuongeza fursa za ajira nchini, viwanda hivvyo ndivyo vitakavyowawezesha wananchi kununua bidhaa kwa bei nafuu tofauti na ilivyo sasa kwa kuwa vitu vingi vinaagizwa kutoka nje ya nchi.

RECENTS
MICHEZO
KUTAKUWA na mtihani na zoezi la utimamu wa mwili (Fitness Test) kwa ajili ya waamuzi wa madaraja ya Tatu na Pili ili kuweza kuwapandisha madaraja kwa mujibu wa utaratibu.
October 09, 2017
Read More
RWANDA na Sudani zimethibitisha kushiriki katika mashindano ya kuogelea ya kanda ya tatu ya Afrika (Cana zone 3) yaliyopangwa kufanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba 19 -21.
September 26, 2017
Read More
HABARI ZA JUU
KITAIFA
SERIKALI haitaweza kuwavumilia watendaji wazembe katika suala zima la uvamizi wa mifugo hususan ng’ombe kutoka katika nchi jirani ya Kenya.
October 16, 2017
Read More
NAIBU Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa ameishauri Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Kilimo ukanda wa Kitropiki (IITA) kuongeza kasi ya utoaji elimu kwa wakulima nchini kuhusu kadhia ya Sumu Kuvu.
October 16, 2017
Read More
WANACHAMA wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) 113 kutoka bara na visiwani wamejitokeza kuwania nafasi ya uenyekiti Taifa katika uchaguzi utakaofanyika mwaka huu, idadi ambayo haijawahi kutokea tangu kuanzishwa kwa umoja huo.
October 16, 2017
Read More
HATIMAYE Katibu Mkuu wa Baraza la Mashirika ya Kiislamu Nchini, Sheikh ISSA PONDA, leo amejisalimisha katika Kituo cha Polisi cha Central, kufuatia agizo la Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam, LAZARO MAMBOSASA.
October 13, 2017
Read More