UHURU FM
Azam FC kuweka kambi ya 10 Uganda.

KLABU ya soka ya Azam FC inatarajiwa kuweka kambi ya siku 10 nchini Uganda kwa ajili ya kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania bara.

Mabingwa hao wa Afrika Mashariki na Kati wanatarajiwa kuondoka nchini Jumapili hii kwa ajili ya kambi hiyo ambayo itakuwa kama sehemu ya maandalizi yao ya mwisho kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa Ligi Kuu.

Azam wenyewe wanatarajia kuanza ligi hiyo ugenini kwa kucheza dhidi ya Ndanda FC mchezo ambao utapigwa katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona Agosti 26 mwaka huu.

Ofisa Habari wa Azam, Jaffar Idd amesema kikosi chao kikiwa nchini humo kinatarajia kucheza mechi nne kubwa za kirafiki dhidi ya KCCA, SC Villa, Vipers na URA.

Idd aliendelea kudai kuwa kikosi hicho kinatarajiwa kurejea nchini Agosti 15 na kufanya maandalizi ya mwisho kabla ya mechi yao ya ufunguzi wa ligi.

RECENTS
MICHEZO
KUTAKUWA na mtihani na zoezi la utimamu wa mwili (Fitness Test) kwa ajili ya waamuzi wa madaraja ya Tatu na Pili ili kuweza kuwapandisha madaraja kwa mujibu wa utaratibu.
October 09, 2017
Read More
RWANDA na Sudani zimethibitisha kushiriki katika mashindano ya kuogelea ya kanda ya tatu ya Afrika (Cana zone 3) yaliyopangwa kufanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba 19 -21.
September 26, 2017
Read More
HABARI ZA JUU
KITAIFA
SERIKALI haitaweza kuwavumilia watendaji wazembe katika suala zima la uvamizi wa mifugo hususan ng’ombe kutoka katika nchi jirani ya Kenya.
October 16, 2017
Read More
NAIBU Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa ameishauri Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Kilimo ukanda wa Kitropiki (IITA) kuongeza kasi ya utoaji elimu kwa wakulima nchini kuhusu kadhia ya Sumu Kuvu.
October 16, 2017
Read More
WANACHAMA wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) 113 kutoka bara na visiwani wamejitokeza kuwania nafasi ya uenyekiti Taifa katika uchaguzi utakaofanyika mwaka huu, idadi ambayo haijawahi kutokea tangu kuanzishwa kwa umoja huo.
October 16, 2017
Read More
HATIMAYE Katibu Mkuu wa Baraza la Mashirika ya Kiislamu Nchini, Sheikh ISSA PONDA, leo amejisalimisha katika Kituo cha Polisi cha Central, kufuatia agizo la Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam, LAZARO MAMBOSASA.
October 13, 2017
Read More