UHURU FM
Bondia Klitschko atangaza kustaafu rasmi ngumi.

BINGWA zamani wa masumbwi ya uzito wa juu, Wladimir Klitschko ametangaza kustaafu rasmi mchezo huo hivyo kuondoa uwezekano wa kurudiana kuzichapa na bondia Anthony Joshua wa Uingereza.

Klitschko mwenye umri wa miaka 41 raia wa Ukraine alipigwa kwa knock out ya raundi ya 11 katika pambano lake dhidi ya Joshua lililofanyika kwenye Uwanja wa Wembley Aprili mwaka huu.

Joshua mwenye umri wa miaka 27 alikuwa akitegemea Klitschko angesaini pamobano la marudiano ambalo lilipangwa kufanyika jijini Las Vegas Novemba 11 mwaka huu.

Klitschko amesema tayari ameshapata kila kitu alichokuwa akitaka na sasa anataka kuanza maisha mapya baada ya mchezo huo wa ngumi.

Bondia huyo mkongwe ambaye alikuwa akishikilia ubingwa wa dunia kutokea mwaka 2006 mpaka 2015 kabla ya kupoteza kwa mwingereza mwingine Tyson Fury, anastaafu akiwa na rekodi nzuri ya kuhsinda mapambano 64 na kupigwa matano pekee.

RECENTS
MICHEZO
KUTAKUWA na mtihani na zoezi la utimamu wa mwili (Fitness Test) kwa ajili ya waamuzi wa madaraja ya Tatu na Pili ili kuweza kuwapandisha madaraja kwa mujibu wa utaratibu.
October 09, 2017
Read More
RWANDA na Sudani zimethibitisha kushiriki katika mashindano ya kuogelea ya kanda ya tatu ya Afrika (Cana zone 3) yaliyopangwa kufanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba 19 -21.
September 26, 2017
Read More
HABARI ZA JUU
KITAIFA
SERIKALI haitaweza kuwavumilia watendaji wazembe katika suala zima la uvamizi wa mifugo hususan ng’ombe kutoka katika nchi jirani ya Kenya.
October 16, 2017
Read More
NAIBU Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa ameishauri Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Kilimo ukanda wa Kitropiki (IITA) kuongeza kasi ya utoaji elimu kwa wakulima nchini kuhusu kadhia ya Sumu Kuvu.
October 16, 2017
Read More
WANACHAMA wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) 113 kutoka bara na visiwani wamejitokeza kuwania nafasi ya uenyekiti Taifa katika uchaguzi utakaofanyika mwaka huu, idadi ambayo haijawahi kutokea tangu kuanzishwa kwa umoja huo.
October 16, 2017
Read More
HATIMAYE Katibu Mkuu wa Baraza la Mashirika ya Kiislamu Nchini, Sheikh ISSA PONDA, leo amejisalimisha katika Kituo cha Polisi cha Central, kufuatia agizo la Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam, LAZARO MAMBOSASA.
October 13, 2017
Read More