UHURU FM
Rais Shein asisitiza haja ya kuandaa viongozi wa michezo

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dokta ALI MOHAMED SHEIN, amesisitiza haja ya kuwaandaa viongozi wa Michezo watakaoendelea kuipa sifa Zanzibar katika sekta hiyo kama ilivyokuwa hapo siku za nyuma.

Dokta SHEIN amesema hayo alipokutana na uongozi wa Wizara ya Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo pamoja na Bodi ya Wakurugenzi ya Baraza la Michezo na Uongozi wa Baraa la Michezo katika vikao vinavyoendelea Ikulu mjini Zanzibar.

Katika vikao hivyo, Dokta SHEIN amesema hatua hiyo itapelekea kuwapata viongozi bora wa michezo hatua ambayo itasaidia hata kupunguza migogoro inayotokea katika vyama na vilabu vya michezo hapa nchini.

Sambamba na hayo, ametoa pongezi kwa uongozi na Bodi ya Baraza la Michezo kwa kuendeleza vyema juhudi za ujenzi wa Viwanja vya Michezo katika Wilaya zote nchini ambapo kwa upande wa Wilaya ya Kusini Kiwanja cha Kitogani kiko hatua za mwisho kumaliza ujenzi wake.

RECENTS
MICHEZO
KUTAKUWA na mtihani na zoezi la utimamu wa mwili (Fitness Test) kwa ajili ya waamuzi wa madaraja ya Tatu na Pili ili kuweza kuwapandisha madaraja kwa mujibu wa utaratibu.
October 09, 2017
Read More
RWANDA na Sudani zimethibitisha kushiriki katika mashindano ya kuogelea ya kanda ya tatu ya Afrika (Cana zone 3) yaliyopangwa kufanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba 19 -21.
September 26, 2017
Read More
HABARI ZA JUU
KITAIFA
SERIKALI haitaweza kuwavumilia watendaji wazembe katika suala zima la uvamizi wa mifugo hususan ng’ombe kutoka katika nchi jirani ya Kenya.
October 16, 2017
Read More
NAIBU Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa ameishauri Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Kilimo ukanda wa Kitropiki (IITA) kuongeza kasi ya utoaji elimu kwa wakulima nchini kuhusu kadhia ya Sumu Kuvu.
October 16, 2017
Read More
WANACHAMA wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) 113 kutoka bara na visiwani wamejitokeza kuwania nafasi ya uenyekiti Taifa katika uchaguzi utakaofanyika mwaka huu, idadi ambayo haijawahi kutokea tangu kuanzishwa kwa umoja huo.
October 16, 2017
Read More
HATIMAYE Katibu Mkuu wa Baraza la Mashirika ya Kiislamu Nchini, Sheikh ISSA PONDA, leo amejisalimisha katika Kituo cha Polisi cha Central, kufuatia agizo la Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam, LAZARO MAMBOSASA.
October 13, 2017
Read More