UHURU FM
Waziri wa Kilimo Zanzibar aitaka TADB kuwawezesha Wakulima

Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar, HAMAD RASHID MOHAMED, ameitaka Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya Tanzania-TADB, kuwezesha Wakulima ili wachangamkie fursa za kuuza Mazao ya Kilimo nje ya nchi ili kuwaongezea kipato.

Waziri HAMAD, ametoa wito huo alipotembelea Banda la TADB katika Viwanja vya Ngongo Mjini Lindi wakati wa Maonesho ya Nane Nane yaliyomalizika hapo jana.

Amesema Tanzania inapata fursa nyingi za Masoko nje ya nchi kwa Mazao mbalimbali ikiwemo Karafuu, Korosho na Mazao ya Mikunde ikiwemo Dengu na Mbaazi zinazotakiwa nchini India na Arabuni.

Kwa mujibu wa Waziri HAMAD, kuna wafanyabiashara wa kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu wanaohitaji zaidi ya Kontena Mbili za Korosho kwa wiki, hivyo Benki hiyo ya Kilimo ina wajibu wa kuwezesha Wakulima ili wanufaike na fursa hizo.

RECENTS
MICHEZO
KUTAKUWA na mtihani na zoezi la utimamu wa mwili (Fitness Test) kwa ajili ya waamuzi wa madaraja ya Tatu na Pili ili kuweza kuwapandisha madaraja kwa mujibu wa utaratibu.
October 09, 2017
Read More
RWANDA na Sudani zimethibitisha kushiriki katika mashindano ya kuogelea ya kanda ya tatu ya Afrika (Cana zone 3) yaliyopangwa kufanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba 19 -21.
September 26, 2017
Read More
HABARI ZA JUU
KITAIFA
SERIKALI haitaweza kuwavumilia watendaji wazembe katika suala zima la uvamizi wa mifugo hususan ng’ombe kutoka katika nchi jirani ya Kenya.
October 16, 2017
Read More
NAIBU Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa ameishauri Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Kilimo ukanda wa Kitropiki (IITA) kuongeza kasi ya utoaji elimu kwa wakulima nchini kuhusu kadhia ya Sumu Kuvu.
October 16, 2017
Read More
WANACHAMA wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) 113 kutoka bara na visiwani wamejitokeza kuwania nafasi ya uenyekiti Taifa katika uchaguzi utakaofanyika mwaka huu, idadi ambayo haijawahi kutokea tangu kuanzishwa kwa umoja huo.
October 16, 2017
Read More
HATIMAYE Katibu Mkuu wa Baraza la Mashirika ya Kiislamu Nchini, Sheikh ISSA PONDA, leo amejisalimisha katika Kituo cha Polisi cha Central, kufuatia agizo la Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam, LAZARO MAMBOSASA.
October 13, 2017
Read More