UHURU FM
Makonda aanza kusikiliza kero za Wananchi

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, PAUL MAKONDA, ameanza kutekeleza agizo la Rais JOHN MAGUFULI, la kumtaka kusikiliza na kuzitafutia ufumbuzi wa kina kero za Wafanyabiashara wadogo wadogo wa Soko la Bunju B, Wilayani Kinondoni.

Katika kutekeleza agizo hilo, jana MAKONDA, amezungumza na Wafanyabiashara hao katika mkutano wa hadhara uliolenga kusikiliza kero zao.

Akiwa katika mkutano huo ameuagiza uongozi wa Mkoa na Wataalamu wa Wilaya ya Kinondoni kuhakikisha Soko hilo linaboreshwa na kuwekewa huduma muhimu ili ziwanufaishe wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla.

Huduma hizo zinazopaswa kuwepo katika Soko hilo ni Maji Safi na Salama, Vyoo, Umeme na Kituo cha Afya.

Juzi, Wafanyabiashara wa Bunju B walisimamisha msafara wa Rais MAGUFULI wakati akitoka Mkoani Tanga, wakimuomba asaidie kusikiliza kero zao ikiwemo ya kutakiwa kuondoka katika Soko hilo, hatua ambayo Rais alisitisha kwa muda agizo hilo, na kuutaka Uongozi wa Mkoa kwenda kuwasikiliza.

 

RECENTS
MICHEZO
KUTAKUWA na mtihani na zoezi la utimamu wa mwili (Fitness Test) kwa ajili ya waamuzi wa madaraja ya Tatu na Pili ili kuweza kuwapandisha madaraja kwa mujibu wa utaratibu.
October 09, 2017
Read More
RWANDA na Sudani zimethibitisha kushiriki katika mashindano ya kuogelea ya kanda ya tatu ya Afrika (Cana zone 3) yaliyopangwa kufanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba 19 -21.
September 26, 2017
Read More
HABARI ZA JUU
KITAIFA
SERIKALI haitaweza kuwavumilia watendaji wazembe katika suala zima la uvamizi wa mifugo hususan ng’ombe kutoka katika nchi jirani ya Kenya.
October 16, 2017
Read More
NAIBU Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa ameishauri Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Kilimo ukanda wa Kitropiki (IITA) kuongeza kasi ya utoaji elimu kwa wakulima nchini kuhusu kadhia ya Sumu Kuvu.
October 16, 2017
Read More
WANACHAMA wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) 113 kutoka bara na visiwani wamejitokeza kuwania nafasi ya uenyekiti Taifa katika uchaguzi utakaofanyika mwaka huu, idadi ambayo haijawahi kutokea tangu kuanzishwa kwa umoja huo.
October 16, 2017
Read More
HATIMAYE Katibu Mkuu wa Baraza la Mashirika ya Kiislamu Nchini, Sheikh ISSA PONDA, leo amejisalimisha katika Kituo cha Polisi cha Central, kufuatia agizo la Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam, LAZARO MAMBOSASA.
October 13, 2017
Read More