UHURU FM
Zuma aponea Chupuchupu kung'olewa Madarakani

Rais wa Afrika Kusini, JACOB ZUMA, ameponea chupuchupu kura ya kutokuwa na Imani naye Bungeni, baada ya Wabunge wengi wa Chama Tawala Cha ANC, kumuunga Mkono.

Jumla ya Wabunge 177 walipiga kura ya kumuondoa madarakani Rais ZUMA, huku Wabunge 198wakipiga kura ya kumuunga mkono na Wabunge Tisa hawakupiga kura .

Wafuasi wa Rais ZUMA wameshangilia ushindi huo kupitia vigelegele na kucheza Densi.

Wabunge 40 wa Chama Tawala cha ANC walipga kura ya kutaka kumng'oa Rais ZUMA.

Lakini ushindi wake ulikuwa mdogo, ikimaanisha kwamba idadi kubwa ya Wabunge kutoka Chama Tawala cha ANC iliunga mkono Muswada huo wa upinzani kumuondoa madarakani.

RECENTS
MICHEZO
KUTAKUWA na mtihani na zoezi la utimamu wa mwili (Fitness Test) kwa ajili ya waamuzi wa madaraja ya Tatu na Pili ili kuweza kuwapandisha madaraja kwa mujibu wa utaratibu.
October 09, 2017
Read More
RWANDA na Sudani zimethibitisha kushiriki katika mashindano ya kuogelea ya kanda ya tatu ya Afrika (Cana zone 3) yaliyopangwa kufanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba 19 -21.
September 26, 2017
Read More
HABARI ZA JUU
KITAIFA
SERIKALI haitaweza kuwavumilia watendaji wazembe katika suala zima la uvamizi wa mifugo hususan ng’ombe kutoka katika nchi jirani ya Kenya.
October 16, 2017
Read More
NAIBU Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa ameishauri Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Kilimo ukanda wa Kitropiki (IITA) kuongeza kasi ya utoaji elimu kwa wakulima nchini kuhusu kadhia ya Sumu Kuvu.
October 16, 2017
Read More
WANACHAMA wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) 113 kutoka bara na visiwani wamejitokeza kuwania nafasi ya uenyekiti Taifa katika uchaguzi utakaofanyika mwaka huu, idadi ambayo haijawahi kutokea tangu kuanzishwa kwa umoja huo.
October 16, 2017
Read More
HATIMAYE Katibu Mkuu wa Baraza la Mashirika ya Kiislamu Nchini, Sheikh ISSA PONDA, leo amejisalimisha katika Kituo cha Polisi cha Central, kufuatia agizo la Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam, LAZARO MAMBOSASA.
October 13, 2017
Read More