UHURU FM
Profesa Mbarawa atoa mwezi mmoja kwa wafanyabiashara wa JNIA

WAZIRI Wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa ametoa Mwezi mmoja kwa wafanyabiashara wanaotoa huduma katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere-JNIA kulipa kodi ya Majengo kama mikataba yao inavyolekeza.

Waziri Mbarawa ametoa agizo hilo leo wakati alipokutana na wafanyabiashara hao ili kujadili changamoto mbalimbali zilizopo na jinsi ya kuzitatua ili kuendelea kutoa huduma bora katika uwanja huo.

Aidha, Profesa Mbarawa ameutaka uongozi wa Mamlaka ya viwanja vya ndege Tanzania-TAA, Kuhakikisha mikataba yote ya upangishaji wa majengo inapitiwa upya na kufanyiwa marekebisho ili thamani ya fedha iendane na wakati huu.

Profesa Mbarawa amewahimiza wafanyabiashara hao kubadilika na kuendana na mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia ili kuweza akuendana na ushindani wa kibiashara uliopo ndani na nje ya nchi.

Ameongeza kuwa Serikali itaendelea kujenga mazingira mazuri kwa wafanyabiashara nchini ili waweze kufanya biashara zao ili kujiingizia kipato binafsi na kukuza pato la Taifa.

Katika hatua nyingine Profesa Mbarawa amekagua sehemu ya kuingilia abiria katika uwanja huo ambapo amesema Serikali itaweka mpango maalum wa muda mfupi kwa wasafiri wanaoenda nje kutotumia muda mrefu katika ujazaji wa fomu wakiwa uwanjani hapo.

Kwa upande Kaimu MKurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania-TAA, Salim Msangi amesema Mamlaka imeshapitia mikataba yote ya wafanyabiashara kiwanjani hapo na hatua inayofata ni kufatilia madeni yote ili kuboresha huduma katika kiwanja hicho. 

RECENTS
MICHEZO
Leo Jumanne Januari 16, 2018 klabu ya Yanga imeingia mkataba wa miaka mitatu (3) na kampuni ya utengenezaji wa vifaa vya michezo ya Macron ambayo makao makuu yake yapo nchini Italy, Macron watakuwa ndio watengenezaji wakuu wa vifaa vyote michezo vya klabu hiyo.
January 16, 2018
Read More
Sekretarieti ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF imewapeleka kwenye kamati ya Maadili viongozi wanne kwa kughushi na udanganyifu.
January 16, 2018
Read More
HABARI ZA JUU
KITAIFA
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Joachim Wangabo, amewatahadharisha wananchi juu ya kuingilia Mhimili wa Mahakama baada ya kupokea malalamiko ya Wakulima 112 waliouza Tani 622 za Mahindi kwa Chama cha Ushirika cha mazao MUZIA AMCOS.
February 21, 2018
Read More
Wananchi katika Vijiji vya Kapeta na Lema Wilayani Ileje Mkoani Songwe, wameiomba Serikali kuufungua Mgodi wa Makaa ya Mawe wa Kiwira ili shughuli zilizokuwa zikifanyika Mgodini hapo zirejea kama kawaida kwa manufaa ya Kijamii na Kiuchumi.
February 21, 2018
Read More
Serikali imepeleka shilingi Bilioni-2.6 katika Jiji la Mwanza kwa ajili ya kugharamia uboreshaji wa Vituo vya Afya ili kuimarisha upatikanaji wa huduma za Afya kwa wananchi.
February 21, 2018
Read More
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, amewataka Watanzania wakiwemo Wakazi wa Mkoa wa Mwanza kuachana na biashara ya Dawa za Kulevya.
February 21, 2018
Read More