UHURU FM
Marekani kupitia USAID yatiliana saini makubaliano ya kutoa fedha za nyongeza Dola Milioni 225 za Marekani kwa Tanzania

SIKU moja baada ya Marekani kutangaza kutoa fedha za nyongeza katika mwaka ujao kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo hapa nchini, nchi hiyo imetiliana saini na Wizara ya Fedha na Mipango makubaliano ya kutoa DolaMilioni 225.

Fedha hizo zitaelekezwa katika sekta mbalimbali zikiwemo Elimu, Afya, Kilimo na Utawala bora.

Hafla ya kutiliana saini makubaliano hayo imefanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam kati ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Doto James na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo la Marekani (USAID) hapa nchini AndyKaras.

Akizungumza baada ya kutiliana saini makubaliano hayo Doto James ameishukuru Marekani kwa kuendeleza uhusiano mzuri uliopona Tanzania na amesema fedha hizo zitasaidia kuimarisha juhudi za Serikali kuwaletea maendeleo wananchi.

Nae Andy Karas amesema Serikali na watu wa Marekani wanafurahishwa na kuendelea kwa ushirikiano mwema kati yao na Serikali ya Tanzania katika maendeleo na ameahidi kuwa ushirikiano huo utadumishwa.

Hafla ya kutiliana saini makubaliano hayo imehudhuriwa na Kaimu Balozi wa Marekani hapan chini Dkt. Inmi Patterson ambaye amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kt. John Magufuli kwa kufanikisha upatikanaji wa fedha hizo. 

RECENTS
MICHEZO
Leo Jumanne Januari 16, 2018 klabu ya Yanga imeingia mkataba wa miaka mitatu (3) na kampuni ya utengenezaji wa vifaa vya michezo ya Macron ambayo makao makuu yake yapo nchini Italy, Macron watakuwa ndio watengenezaji wakuu wa vifaa vyote michezo vya klabu hiyo.
January 16, 2018
Read More
Sekretarieti ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF imewapeleka kwenye kamati ya Maadili viongozi wanne kwa kughushi na udanganyifu.
January 16, 2018
Read More
HABARI ZA JUU
KITAIFA
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Joachim Wangabo, amewatahadharisha wananchi juu ya kuingilia Mhimili wa Mahakama baada ya kupokea malalamiko ya Wakulima 112 waliouza Tani 622 za Mahindi kwa Chama cha Ushirika cha mazao MUZIA AMCOS.
February 21, 2018
Read More
Wananchi katika Vijiji vya Kapeta na Lema Wilayani Ileje Mkoani Songwe, wameiomba Serikali kuufungua Mgodi wa Makaa ya Mawe wa Kiwira ili shughuli zilizokuwa zikifanyika Mgodini hapo zirejea kama kawaida kwa manufaa ya Kijamii na Kiuchumi.
February 21, 2018
Read More
Serikali imepeleka shilingi Bilioni-2.6 katika Jiji la Mwanza kwa ajili ya kugharamia uboreshaji wa Vituo vya Afya ili kuimarisha upatikanaji wa huduma za Afya kwa wananchi.
February 21, 2018
Read More
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, amewataka Watanzania wakiwemo Wakazi wa Mkoa wa Mwanza kuachana na biashara ya Dawa za Kulevya.
February 21, 2018
Read More