UHURU FM
Dkt.shein akutana na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola

JUMUIYA ya Madola imeahidi kuendelea kuiunga mkono Zanzibar katika kuimarisha sekta mbali mbali za maendeleo kama ilivyo kwa wanachama wengine wote 52 wa Jumiya hiyo.

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola  Baroness  Patricia Scotland aliyasema hayo leo wakati alipofanya mazungumzo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein Ikulu mjini Zanzibar.

Katika maelezo yake Katibu Mkuu huyo alieleza kuwa Jumuiya ya Madola inaendelea kutekeleza mipango na mikakati kabambe ambayo imeiweka kwa wanancha wake ikiwemo Tanzania ambapo Zanzibar pia, ni miongoni mwao.

Baroness  Scotland alitumia fursa hiyo kutoa pongezi kwa Rais Dk. Shein kwa juhudi kubwa anazozichukua katika kuhakikisha Zanzibar inakuza uchumi na kuimarisha amani na utulivu na kusisitiza kuwa Jumuiya anayoiongoza haitokuwa nyuma kumuunga mkono.

Aidha, Baroness  Scotland alimueleza Dk. Shein miongoni mwa mipango ya Jumuiya hiyo kwa nchi wanachama wake wote 52 ikiwa ni pamoja na kuongeza fursa katika sekta ya biashara nan uchumi, kuwasaidia wanawake, vijana, upatikanaji ajira kwa vijana, elimu, kutunza mazingira, uwezeshaji na mengineyo.

Aliongeza kuwa uchumi kwa nchi wanachama wa Jumuiya hiyo umekuwa ukiimarika kwa kiasi kikubwa kwa zile nchi za Bara la Afrika na hata nchi za Bara la Asia uchumi wake umeimarika kwa asilimia 5 hadi asilimia 8.

RECENTS
MICHEZO
Leo Jumanne Januari 16, 2018 klabu ya Yanga imeingia mkataba wa miaka mitatu (3) na kampuni ya utengenezaji wa vifaa vya michezo ya Macron ambayo makao makuu yake yapo nchini Italy, Macron watakuwa ndio watengenezaji wakuu wa vifaa vyote michezo vya klabu hiyo.
January 16, 2018
Read More
Sekretarieti ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF imewapeleka kwenye kamati ya Maadili viongozi wanne kwa kughushi na udanganyifu.
January 16, 2018
Read More
HABARI ZA JUU
KITAIFA
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Joachim Wangabo, amewatahadharisha wananchi juu ya kuingilia Mhimili wa Mahakama baada ya kupokea malalamiko ya Wakulima 112 waliouza Tani 622 za Mahindi kwa Chama cha Ushirika cha mazao MUZIA AMCOS.
February 21, 2018
Read More
Wananchi katika Vijiji vya Kapeta na Lema Wilayani Ileje Mkoani Songwe, wameiomba Serikali kuufungua Mgodi wa Makaa ya Mawe wa Kiwira ili shughuli zilizokuwa zikifanyika Mgodini hapo zirejea kama kawaida kwa manufaa ya Kijamii na Kiuchumi.
February 21, 2018
Read More
Serikali imepeleka shilingi Bilioni-2.6 katika Jiji la Mwanza kwa ajili ya kugharamia uboreshaji wa Vituo vya Afya ili kuimarisha upatikanaji wa huduma za Afya kwa wananchi.
February 21, 2018
Read More
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, amewataka Watanzania wakiwemo Wakazi wa Mkoa wa Mwanza kuachana na biashara ya Dawa za Kulevya.
February 21, 2018
Read More