UHURU FM
Wananchi wataka zoezi la kupima afya bure liongezewe muda

WAKATI kesho ikiwa ni Siku ya mwisho ya Upimaji wa Afya Bure katika kwa wakazi wa Mkoa wa Dar es salaam katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, Wakazi wa Mkoa huo, wameomba huduma hiyo iongezewe muda kutokana na idadi kubwa ya watu kuendelea kujitokeza na kuhofia baadhi yao kukosa huduma.

Uhuru Fm imeshuhudia idadi kubwa ya watu wakipimwa magonjwa ya Moyo, Figo, Saratani na Macho, huku utaratibu wa utoaji wa huduma ukiwa ni mzuri.

Zoezi hilo ambalo linaratibiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, PAUL MAKONDA kwa kushirikiana pia na Mradi wa Uhuru Fm wa Gusa Maisha Yao, limehusisha Wataalamu wa Afya zaidi ya 200. 

RECENTS
MICHEZO
KOCHA wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars Salum Mayanga ameita kikosi cha wacheza 24 watakaoingia kambini kwa ajili ya mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Benin.
October 24, 2017
Read More
Mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya Young Africans na Simba utafanyika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam kama ilivyotangazwa awali. Hakuna mabadiliko.
October 23, 2017
Read More
HABARI ZA JUU
KITAIFA
BUNGE limepitisha marekebisho ya sheria ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya wa mwaka 2017 yenye lengo la kuboresha utekelezaji wa sheria na kuondoa upungufu uliojitokeza wakati wa kuitumia sheria hiyo.
November 17, 2017
Read More
MAAFISA kutoka Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Abeid Amani Karume cha Zanzibar (AAKIA), wamefurahishwa na namna ulinzi na usalama wa abiria na mali zao unavyofanywa kwenye Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), imeelezwa.
November 15, 2017
Read More
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan leo amefungua mkutano wa pili wa Biashara, Ujasiriamali na Maonyesho wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ulioandaliwa na Baraza la Biashara la Afrika Mashariki.
November 14, 2017
Read More
KATIKA kuhakikisha Vijana wengi zaidi wanapata Elimu ya Ufundi, Serikali inaendelea na Mpango wake wa Ujenzi wa Vyuo vya Ufundi 43 katika Wilaya mbalimbali nchini.
November 14, 2017
Read More