UHURU FM
Serikali yataifisha Almasi iliyokamatwa JKIA

SERIKALI imetangaza kutaifisha Madini ya Almasi yenye uzito wa kilo 29 yaliyokuwa yasafirishwe nchini Ubelgiji kwa ajili ya Mauzo.

Uamuzi huo wa serikali umetangazwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dokta PHILIP MIPANGO, muda mfupi wa kuyashuhudia Madini yao katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini dare s salaam.

Hatua hiyo ya serikali imekuja kufuatia Kamati Maalumu ya Wataalamu uliyoundwa na serikali kuchunguza Madini ya Almas yaliyokamatwa hivi karibuni katika Uwanja huo wa Ndege kubaini kuwa kulikuwa na udanganyifu mkubwa wa kiasi cha Madini, ambapo awali ilidaiwa kuwa yalikuwa na uzito wa Kilo 14 kumbe ni Kilo 29.

Katika Madini hayo yalikuwa yasafirishwe kwenda nchini Ubelgiji serikali ingepoteza mapato ya kiasi cha shilingi Bilioni-32.

Kufuatia udanganyifu huo, Waziri wa Fedha na Mipango, Dokta MIPANGO, ameagiza watumishi wote wa serikali waliopo katika Mgodi wa Almas wa Mwadui Shinyanga Wakamate pamoja na mali zao kuorodheshwe.

Pia Waziri MPANGO, ameagiza kuanzia sasa Madini yote yakaguliwe Mgodini pamoja na Uwanja wa Ndege ili kuepusha upootevu wa rasilimali za Watanzania.

Mapema Kiongozi wa Jopo la Wataalamu waliofanya tathimini ya Madini ya Almasi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam pamoja na mambo mengine, Profesa MRUMA, amependekeza mali zote za wahusika zitaifishwe.

RECENTS
MICHEZO
KOCHA wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars Salum Mayanga ameita kikosi cha wacheza 24 watakaoingia kambini kwa ajili ya mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Benin.
October 24, 2017
Read More
Mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya Young Africans na Simba utafanyika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam kama ilivyotangazwa awali. Hakuna mabadiliko.
October 23, 2017
Read More
HABARI ZA JUU
KITAIFA
BUNGE limepitisha marekebisho ya sheria ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya wa mwaka 2017 yenye lengo la kuboresha utekelezaji wa sheria na kuondoa upungufu uliojitokeza wakati wa kuitumia sheria hiyo.
November 17, 2017
Read More
MAAFISA kutoka Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Abeid Amani Karume cha Zanzibar (AAKIA), wamefurahishwa na namna ulinzi na usalama wa abiria na mali zao unavyofanywa kwenye Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), imeelezwa.
November 15, 2017
Read More
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan leo amefungua mkutano wa pili wa Biashara, Ujasiriamali na Maonyesho wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ulioandaliwa na Baraza la Biashara la Afrika Mashariki.
November 14, 2017
Read More
KATIKA kuhakikisha Vijana wengi zaidi wanapata Elimu ya Ufundi, Serikali inaendelea na Mpango wake wa Ujenzi wa Vyuo vya Ufundi 43 katika Wilaya mbalimbali nchini.
November 14, 2017
Read More