UHURU FM
Wahalifu wavamia ofisi za mawakili wa Prime

WATU wanane wanaodaiwa kuwa ni wahalifu wamevamia Jengo la Prime House lililopo Mtaa wa Tambaza, Upanga jijini Dar es salaam, na kufanya uharibifu wa mali za Wapangaji.

Jengo la Prime House lina ghorofa Tano lipo jirani na Ofisi za Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa-TAKUKURU, Manispaa ya Ilala.

Barabara ya kuingia eneo hilo ilifungwa kwa muda na Polisi ambao walitumia Magari yao kuziba njia na kuweka uzio wa Utepe wa Rangi ya Njano.        Jengo la Prime House lina Ofisi za Kampuni mbalimbali zikiwemo za Mawakili, Duka la Dawa na sehemu ya kufanya mazoezi GYM.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala, SALUM HAMDUNI, amethibitisha kuvamiwa na kuvunjwa kwa Jengo hilo lenye Ofisi mbalimbali ikiwamo Ofisi ya Mawakili wa Prime Lawyers.

Kamanda HAMDUNI amesema Polisi wako eneo la tukio kwa uchunguzi wa awali ili kujua Ofisi zilizoathirika kutokana na tukio hilo na kusudio la wavamizi huo.

Akizungumzia tukio hilo mmoja wa Mawakili wa Prime Lawyers, amedai kuwa mlinzi wa Jengo hilo amekutwa amefungwa Kamba Miguuni na Mikononi pamoja na Mdomo kwa kutumia Plasta.

Inadaiwa uvamizi huo umefanyika Saa Nane Usiku wa kuamkia leo.

RECENTS
MICHEZO
KAMATI ya Utendaji ya Chama Cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), iliyokutana Dar es Salaam jana Septemba 7, 2017, imepanga Uchaguzi Mkuu wa chama hicho ufanyike Novemba 5, mwaka huu.
September 08, 2017
Read More
WINGA wa Klabu ya Azam FC Joseph Kimwaga, anatarajia kukaa nje ya dimba kwa muda miezi minne baada ya kubainika ya kuwa amechanika mtulinga wa kati ‘meniscus’ kwenye goti lake la mguu wa kushoto.
September 05, 2017
Read More
HABARI ZA JUU
KITAIFA
SERIKALI imekitaka Chuo Cha Utumishi wa Umma Tanzani (TPSC) kufanya tafiti, kutoa mafunzo na kutoa ushauri unaolenga kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii kwa sasa ikiwamo umasikini.
September 25, 2017
Read More
MAKAMU wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Hassan Suluhu leo amefungua mkutano Mkuu wa Mwaka wa chama cha majaji na mahakimu wa Jumuiya ya Madola katika ukumbi wa mkutano wa Benki Kuu (B.O.T) jijini Dar es Salaam.
September 25, 2017
Read More
Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji wa Serikali, Dokta HASSAN ABBAS, amesema hakuna masharti yaliyowekwa na serikali ili Mbunge wa Singida Mashariki, TUNDU LISSU apatiwe matibabu na kwamba kinachosubiriwa ni maombi ili kugharamia matibabu yake.
September 25, 2017
Read More
WAFANYAKAZI nchini wameshauriwa kupima afya zao mara tu wanapostaafu ili kujihakikishia ikiwa hawajaathirika na kazi ambazo wamekuwa wakizifanya.
September 22, 2017
Read More