UHURU FM
Zitto, Kubenea kuhojiwa Kamati ya Maadili

SPIKA wa Bunge, Job Ndugai, ameiagiza Kamati ya Maadili, Kinga na Madaraka ya Bunge chini ya Mwenyekiti wake, George Mkuchika, kuwaita na kuwahoji Wabunge Wawili, SAID KUBENEA na ZITTO KABWE kuhusu tuhuma zinazowakabili.

Aidha, ameiagiza pia Kamati ya Ulinzi, Usalama na Mambo ya Nje inayoongozwa na Mwenyekiti ADAD RAJAB, kumuita KUBENEA, popote alipo ili kesho aripoti katika Kamati hiyo na kujibu tuhuma zake.

KUBENEA ambaye ni Mbunge wa Ubungo, anatuhumiwa kutumia Kanisa la Ufufuko na Uzima, kutoa tuhuma dhidi ya Spika kuwa amedanganya idadi chache ya Risasi alizopigwa Mbunge wa Singida Mashariki TUNDU LISSU lakini pia ameonekana anajua zaidi tatizo lililomtokea LISSU na hivyo atoe ushahidi ili kusaidia uchunguzi unaoendelea.

Pia Spika wa Bunge, amesema ZITTO ambaye ni Mbunge wa Kigoma Mjini, anatuhumiwa kumtuhumu Spika kuwa amekosea kwenye utaratibu alioutumia katika kushughulikia Ripoti Mbili za Almas na Tanzanite na kusema ripoti hizo zilitakiwa zipelekwe Bungeni.

Spika wa Bunge amefafanua kuwa Kamati mbalimbali zinaundwa kutokana na Kanuni tofauti tofauti na Kamati zile aliunda yeye na sio kwamba ziliundwa na Wabunge hivyo kupelekwa Bungeni sio lazima.

Wakati huo huo, Spika wa Bunge, ameeleza hali ya Mbunge LISSU na kusema anaendelea vizuri na matibabu na kwa mujibu wa taarifa wanazopata hali yake inatia Moyo na kwamba kinachofanyika sasa ni upasuaji ambao wanaufanya kwa Awamu.

 

 

RECENTS
MICHEZO
KOCHA wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars Salum Mayanga ameita kikosi cha wacheza 24 watakaoingia kambini kwa ajili ya mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Benin.
October 24, 2017
Read More
Mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya Young Africans na Simba utafanyika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam kama ilivyotangazwa awali. Hakuna mabadiliko.
October 23, 2017
Read More
HABARI ZA JUU
KITAIFA
BUNGE limepitisha marekebisho ya sheria ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya wa mwaka 2017 yenye lengo la kuboresha utekelezaji wa sheria na kuondoa upungufu uliojitokeza wakati wa kuitumia sheria hiyo.
November 17, 2017
Read More
MAAFISA kutoka Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Abeid Amani Karume cha Zanzibar (AAKIA), wamefurahishwa na namna ulinzi na usalama wa abiria na mali zao unavyofanywa kwenye Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), imeelezwa.
November 15, 2017
Read More
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan leo amefungua mkutano wa pili wa Biashara, Ujasiriamali na Maonyesho wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ulioandaliwa na Baraza la Biashara la Afrika Mashariki.
November 14, 2017
Read More
KATIKA kuhakikisha Vijana wengi zaidi wanapata Elimu ya Ufundi, Serikali inaendelea na Mpango wake wa Ujenzi wa Vyuo vya Ufundi 43 katika Wilaya mbalimbali nchini.
November 14, 2017
Read More