UHURU FM
Maandamano mabaya yashuhudiwa Ethiopia

Takriban watu 2 wameuawa kwenye maandamano nchini Ethiopia.

Zaidi ya watu 600 wamehama wakati wa makabiliano ya siku ya Jumanne katika miji iliyo mashariki mwa nchi

Waandamanaji wanawalaumu polisi kwa kutekeleza mauaji na ukiukaji mwingine wa haki za binadamu dhidi ya watu wa Oromo.

Serikali imesema kuwa ghasia hizo zimesabaishwa na mzozo wa mpaka kati ya watu wa Oromo na majirani zao walio eneo la Somalia nchini Ethiopia.

Serikali imesema kuwa sasa imetuma jeshi kwenda kufanya kile kile ilichokitaja kuwa kutwaa silaha

Mzozo umekuwa ukiendelea kwa miezi kadhaa lakini umechaha wiki hii na kugeuka kuwa makabiliano makali.

Mwezi Agosti serikali iliondoa amri ya tahadhari iliyowekwa kufuatia maandamano ya zaidi ya miaka miwili yanayoipinga serikali.

Source: BBC

RECENTS
MICHEZO
KOCHA wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars Salum Mayanga ameita kikosi cha wacheza 24 watakaoingia kambini kwa ajili ya mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Benin.
October 24, 2017
Read More
Mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya Young Africans na Simba utafanyika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam kama ilivyotangazwa awali. Hakuna mabadiliko.
October 23, 2017
Read More
HABARI ZA JUU
KITAIFA
BUNGE limepitisha marekebisho ya sheria ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya wa mwaka 2017 yenye lengo la kuboresha utekelezaji wa sheria na kuondoa upungufu uliojitokeza wakati wa kuitumia sheria hiyo.
November 17, 2017
Read More
MAAFISA kutoka Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Abeid Amani Karume cha Zanzibar (AAKIA), wamefurahishwa na namna ulinzi na usalama wa abiria na mali zao unavyofanywa kwenye Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), imeelezwa.
November 15, 2017
Read More
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan leo amefungua mkutano wa pili wa Biashara, Ujasiriamali na Maonyesho wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ulioandaliwa na Baraza la Biashara la Afrika Mashariki.
November 14, 2017
Read More
KATIKA kuhakikisha Vijana wengi zaidi wanapata Elimu ya Ufundi, Serikali inaendelea na Mpango wake wa Ujenzi wa Vyuo vya Ufundi 43 katika Wilaya mbalimbali nchini.
November 14, 2017
Read More