UHURU FM
Rais Dkt Magufuli aivunja KDA

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta John Magufuli, amevunja Mamlaka ya Usimamizi wa Mji Mdogo wa Kigamboni-KDA, ambapo kuanzia sasa shughuli zote zilizokuwa zikifanywa na Mamlaka hiyo zitafanywa Manispaa ya Kigamboni.

Hatua hiyo imekuja kutokana na Mkanganyiko wa kimajukumu uliokuwepo kati ya KDA na Manispaa ya Kigamboni.

Uamuzi huo umetangazwa leo na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, WILIAM LUKUVI, alipotembelea Kigamboni na kuzungumza na wananchi pamoja na viongozi wa Manispaa ya Kigamboni.

Hata hivyo, Waziri LUKUVI ametoa miezi Sita kwa watendaji wa KDA kukamilisha makabidhiano ya Nyaraka na wao kuripoti kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni.

Awali, Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, HASHIM MGANDILWA, amesema mgongano wa usimamizi wa Ardhi Kigamboni ulisababisha migogoro mingi ya Ardhi.

 

WAKATI HUO HUO,

Serikali imelifuta Shamba la Mfanyabiashara YUSUF MANJI lenye ukubwa wa Hekari 714.

Uamuzi huo wa serikali umetangazwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, WILLIAM LUKUVI, huku akisema Shamba hilo litapangiwa matumizi mengine.

Amesema Shamba jingine la Kampuni ya Amadori lenye ukubwa wa Hekari 5,400 pia limefutwa na kwamba Mashamba hayo sasa yako mikononi mwa Serikali na yatapangiwa matumizi mengine.

Pia Waziri LUKUVI amewaonya wananchi wasivamie maeneo hayo kwa kuwa watakaokamatwa watashitakiwa.

RECENTS
MICHEZO
KOCHA wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars Salum Mayanga ameita kikosi cha wacheza 24 watakaoingia kambini kwa ajili ya mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Benin.
October 24, 2017
Read More
Mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya Young Africans na Simba utafanyika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam kama ilivyotangazwa awali. Hakuna mabadiliko.
October 23, 2017
Read More
HABARI ZA JUU
KITAIFA
BUNGE limepitisha marekebisho ya sheria ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya wa mwaka 2017 yenye lengo la kuboresha utekelezaji wa sheria na kuondoa upungufu uliojitokeza wakati wa kuitumia sheria hiyo.
November 17, 2017
Read More
MAAFISA kutoka Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Abeid Amani Karume cha Zanzibar (AAKIA), wamefurahishwa na namna ulinzi na usalama wa abiria na mali zao unavyofanywa kwenye Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), imeelezwa.
November 15, 2017
Read More
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan leo amefungua mkutano wa pili wa Biashara, Ujasiriamali na Maonyesho wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ulioandaliwa na Baraza la Biashara la Afrika Mashariki.
November 14, 2017
Read More
KATIKA kuhakikisha Vijana wengi zaidi wanapata Elimu ya Ufundi, Serikali inaendelea na Mpango wake wa Ujenzi wa Vyuo vya Ufundi 43 katika Wilaya mbalimbali nchini.
November 14, 2017
Read More