UHURU FM
Almasi iliyopatikana nchini Botswana yauzwa kwa dola milioni 53

ALMASI yenye haijakatwa ya ukubwa wa mpira wa tenisi, iliyopatikana kwenye mgodi wa Korowe nchini Botswana mwezi Novemba mwaka 2015, imeuzwa na kampuni yenye makao yake nchini Canada ya Lucara Diamond kwa kima cha dola milioni 53

Almasi hiyo yenye karati 1,109 ambayo kwa sasa ndiyo kubwa zaidi ambayo bado haijakatwa duniani, ilinunuliwa na kampuni ya Uingereza ya Graff Diamonds kwa dola 47,777 kwa kila karati na sasa itakatwa.

Kampuni ya Canada awali ilijaribu kuiuza almasi hiyo kwenye mnada mwezi Juni mwaka 2016, lakini haikupata bei ilikuwa inahitajika.

Almasi hiyo kwa jina Lesedi La Rona au mwangaza wetu kwa lugha ya taifa nchini Botswana inatajwa kuwa ya miaka bilioni 2.5 hadi bilioni 3.

Kampuni ya Laurence Graff, ilisema kuwa ni hashima kubwa kuwa sasa inamiliki almasi hiyo.

Source: BBC

RECENTS
MICHEZO
KUTAKUWA na mtihani na zoezi la utimamu wa mwili (Fitness Test) kwa ajili ya waamuzi wa madaraja ya Tatu na Pili ili kuweza kuwapandisha madaraja kwa mujibu wa utaratibu.
October 09, 2017
Read More
RWANDA na Sudani zimethibitisha kushiriki katika mashindano ya kuogelea ya kanda ya tatu ya Afrika (Cana zone 3) yaliyopangwa kufanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba 19 -21.
September 26, 2017
Read More
HABARI ZA JUU
KITAIFA
SERIKALI haitaweza kuwavumilia watendaji wazembe katika suala zima la uvamizi wa mifugo hususan ng’ombe kutoka katika nchi jirani ya Kenya.
October 16, 2017
Read More
NAIBU Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa ameishauri Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Kilimo ukanda wa Kitropiki (IITA) kuongeza kasi ya utoaji elimu kwa wakulima nchini kuhusu kadhia ya Sumu Kuvu.
October 16, 2017
Read More
WANACHAMA wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) 113 kutoka bara na visiwani wamejitokeza kuwania nafasi ya uenyekiti Taifa katika uchaguzi utakaofanyika mwaka huu, idadi ambayo haijawahi kutokea tangu kuanzishwa kwa umoja huo.
October 16, 2017
Read More
HATIMAYE Katibu Mkuu wa Baraza la Mashirika ya Kiislamu Nchini, Sheikh ISSA PONDA, leo amejisalimisha katika Kituo cha Polisi cha Central, kufuatia agizo la Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam, LAZARO MAMBOSASA.
October 13, 2017
Read More