UHURU FM
Waziri Mwijage ataka uvuvi haramu ukomeshwe Kagera

WAZIRI wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, amewataka Wavuvi Mkoani Kagera kuachana na Uvuvi Haramu kwani siku zao zinahesabika.

Waziri MWIJAGE, ametoa kauli hiyo Wilayani Muleba alipotembea Kisiwa cha Bumbire kilichomo Ziwa Victoria.

Amesema kwa sasa Serikali imeweka mikakati madhubuti ya kupambana na Uvuvi haramu katika maeneo mbalimbali, ambapo wataanzaa kuwawajibishwa watendaji wa Vijiji kwa kuwasimamisha kazi endapo watashindwa kudhibiti uvuvi haramu na kuendelea kuwakumbatia Wavuvi haramu.

Waziri MWIJAGE ameyataja maeneo ambaye yanaoongoza kwa Uvuvi haramu kuwa ni Chato, Mganza na Kimwani, na hivyo kuwataka viongozi wa vijiji kuchukua hatua kukabiliana na Wavuvi haramu.

Wakati huo huo, Wavuvi wametakiwa kutumia fursa ya kuuza dagaa wasio na mchana kwa shilingi Elfu-35, ambapo Dagaa wenye Mchanga wanauzwa kilo shilingi Elfu-7.

RECENTS
MICHEZO
KUTAKUWA na mtihani na zoezi la utimamu wa mwili (Fitness Test) kwa ajili ya waamuzi wa madaraja ya Tatu na Pili ili kuweza kuwapandisha madaraja kwa mujibu wa utaratibu.
October 09, 2017
Read More
RWANDA na Sudani zimethibitisha kushiriki katika mashindano ya kuogelea ya kanda ya tatu ya Afrika (Cana zone 3) yaliyopangwa kufanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba 19 -21.
September 26, 2017
Read More
HABARI ZA JUU
KITAIFA
SERIKALI haitaweza kuwavumilia watendaji wazembe katika suala zima la uvamizi wa mifugo hususan ng’ombe kutoka katika nchi jirani ya Kenya.
October 16, 2017
Read More
NAIBU Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa ameishauri Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Kilimo ukanda wa Kitropiki (IITA) kuongeza kasi ya utoaji elimu kwa wakulima nchini kuhusu kadhia ya Sumu Kuvu.
October 16, 2017
Read More
WANACHAMA wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) 113 kutoka bara na visiwani wamejitokeza kuwania nafasi ya uenyekiti Taifa katika uchaguzi utakaofanyika mwaka huu, idadi ambayo haijawahi kutokea tangu kuanzishwa kwa umoja huo.
October 16, 2017
Read More
HATIMAYE Katibu Mkuu wa Baraza la Mashirika ya Kiislamu Nchini, Sheikh ISSA PONDA, leo amejisalimisha katika Kituo cha Polisi cha Central, kufuatia agizo la Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam, LAZARO MAMBOSASA.
October 13, 2017
Read More