UHURU FM
Nyumba ya mchezaji aliyeshindwa kufunga mabao yavamiwa na mashabiki Zambia

POLISI nchini Zambia wamewakamata mashabiki watano kwa madai ya kuvamia nyumba ya mchezaji wa soka wa timu ya taifa ya nchi hiyo Alex N'gonga.

Mashabiki hao walishikwa na hasira kufyatia Ng'onga kukosa nafasi nyingi za wazi za kufunga kwenye mchezo wao muhimu wa kufuzu michuano ya Kombe la Dunia ambao Nigeria walishinda bao 1-0.

Kwa mujibu wa taarifa ya polisi mashabiki hao walitoa hasira zao kwa kuvamia nyumba yake iliyopo kwenye mji wa Kitwe na kuitupia mawe.

Kushindwa kwa Zambia kuliinyima fursa ya kufuzu kwa michuano hiyo itakayofanyika Urusi mwakani.

Nigeria wao walifuzu kwa ushindi huo.

Source: BBC

RECENTS
MICHEZO
KOCHA wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars Salum Mayanga ameita kikosi cha wacheza 24 watakaoingia kambini kwa ajili ya mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Benin.
October 24, 2017
Read More
Mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya Young Africans na Simba utafanyika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam kama ilivyotangazwa awali. Hakuna mabadiliko.
October 23, 2017
Read More
HABARI ZA JUU
KITAIFA
BUNGE limepitisha marekebisho ya sheria ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya wa mwaka 2017 yenye lengo la kuboresha utekelezaji wa sheria na kuondoa upungufu uliojitokeza wakati wa kuitumia sheria hiyo.
November 17, 2017
Read More
MAAFISA kutoka Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Abeid Amani Karume cha Zanzibar (AAKIA), wamefurahishwa na namna ulinzi na usalama wa abiria na mali zao unavyofanywa kwenye Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), imeelezwa.
November 15, 2017
Read More
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan leo amefungua mkutano wa pili wa Biashara, Ujasiriamali na Maonyesho wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ulioandaliwa na Baraza la Biashara la Afrika Mashariki.
November 14, 2017
Read More
KATIKA kuhakikisha Vijana wengi zaidi wanapata Elimu ya Ufundi, Serikali inaendelea na Mpango wake wa Ujenzi wa Vyuo vya Ufundi 43 katika Wilaya mbalimbali nchini.
November 14, 2017
Read More