UHURU FM
Uhuru FM kupitia kampeni ya Gusa Maisha Yao yabisha hodi Sober House

UHURU FM kupitia kampeni ya GUSA MAISHA YAO imeendelea kutoa misaada mbalimbali,ambapo leo imetembelea na kutoa msaada katika kituo cha Kutunza Waraibu wa Dawa za Kulevya cha PilliMissana Foundation Kilichopo Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Afisa Uhusiano wa Uhuru FM ARNOLD DOMINIC amesema ni Jukumu la Taifa kwa ujumla kurudisha faraja iliyopotea kwa vijana ambao ni waraibu wa dawa za kulevya,ambapo Uhuru Fm imeamua Kugusa Maisha ya vijana hao kwa kuwa ni watu muhimu katika maendeleo ya Taifa.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo hicho PILLI MISSANA ameishukuru UHURU FM kwa kutoa msaada huo,na kusema msaada huo utaendelea kutumika katika harakati za kuwakomboa vijana hao katika matumizi ya dawa za kulevya.

Pamoja na msaada huo,Uhuru Fm imezungumza na baadhi ya waraibu wa dawa za kulevya ambapo mmoja kati yao ni Mwanamuziki wa Bongo Fleva anayejulikana kwajina la HAWA NITAREJEA na hapa anazungumzia changamoto alizokuutana nazo hadi kupelekea kutumia dawa za kulevya.

Kwa kuwa tunawajali na kuwapenda ndugu zetu hawa ambao no waraibu wa dawa za kulevya,tutaendelea kuwaombea dua ili warejee katika hali zao za kawaida ili waguse maisha ya vijana wengi waliopoteza matumaini.

 Kampeni hii ya GUSA MAISHA YAO bado inaendelea ambapo Oktoba 12 tutagusa maisha kwa uchangiaji wa Damu Salama,utakaofanyika katika Ofisi Kuu za CCM mkoa wa Dar es Salaam,Lumumba jijini Dar es Salaam.

RECENTS
MICHEZO
KUTAKUWA na mtihani na zoezi la utimamu wa mwili (Fitness Test) kwa ajili ya waamuzi wa madaraja ya Tatu na Pili ili kuweza kuwapandisha madaraja kwa mujibu wa utaratibu.
October 09, 2017
Read More
RWANDA na Sudani zimethibitisha kushiriki katika mashindano ya kuogelea ya kanda ya tatu ya Afrika (Cana zone 3) yaliyopangwa kufanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba 19 -21.
September 26, 2017
Read More
HABARI ZA JUU
KITAIFA
SERIKALI haitaweza kuwavumilia watendaji wazembe katika suala zima la uvamizi wa mifugo hususan ng’ombe kutoka katika nchi jirani ya Kenya.
October 16, 2017
Read More
NAIBU Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa ameishauri Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Kilimo ukanda wa Kitropiki (IITA) kuongeza kasi ya utoaji elimu kwa wakulima nchini kuhusu kadhia ya Sumu Kuvu.
October 16, 2017
Read More
WANACHAMA wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) 113 kutoka bara na visiwani wamejitokeza kuwania nafasi ya uenyekiti Taifa katika uchaguzi utakaofanyika mwaka huu, idadi ambayo haijawahi kutokea tangu kuanzishwa kwa umoja huo.
October 16, 2017
Read More
HATIMAYE Katibu Mkuu wa Baraza la Mashirika ya Kiislamu Nchini, Sheikh ISSA PONDA, leo amejisalimisha katika Kituo cha Polisi cha Central, kufuatia agizo la Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam, LAZARO MAMBOSASA.
October 13, 2017
Read More