UHURU FM
Wafanyakazi na Wadau mbalimbali wa Uhuru FM kupitia kampeni ya Gusa Maisha Yao kesho kuchangia damu

KATIKA kuelekea kumbukumbu ya miaka Kumi na Minane ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, Kituo cha Uhuru FM kupitia Kampeni yake ya Gusa Maisha Yao, kimefanikiwa Kugusa Maisha ya baadhi ya Watanzania wenye uhitaji kwa kutoa misaada ya Vyakula na vitu mbalimbali.

Tangu kuanza kwa Kampeni ya Gusa Maisha Yao, Kituo cha Uhuru FM kimetembelea Vituo vyenye uhitaji wa Faraja, ambapo kimetoa msaada wa vitu vikiwemo Vyakula katika Kituo cha Watoto Yatima-Chakuwama, na Kituo cha Tumaini la Maisha cha Watoto wenye Maradhi ya Saratani kilichopo Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Misaada hiyo iliyotolewa na Wasikilizaji pamoja na wadau mbalimbali imepelekwa pia katika Kituo cha Vijana walioathirika na Dawa za Kulevya, Soba House kilichopo Kigamboni jijini Dar es salaam.

Kesho, Alhamis, Wafanyakazi wa Uhuru FM, kwa kushirikiana na wadau mbalimbali watajitolea kutoa Damu katika zoezi litakalofanyika kwenye Viwanja vya Jengo la CCM, Mkoa wa Dar es salaam, Tandika Sokoni, pamoja na Kiwanda cha Nguo Urafiki.

Kilele cha Kampeni ya Gusa Maisha Yao awamu ya kwanza kitafanyika Jumamosi hii katika Viwanja vya MwembeYanga, Temeke, jijini Dar es salaam kwa kuhusisha Tamasha la Michezo na Burudani ya Muziki kutoka kwa Wasanii mbalimbali nchini kuanzia Majira ya Asubuhi hadi Jioni.

RECENTS
MICHEZO
KUTAKUWA na mtihani na zoezi la utimamu wa mwili (Fitness Test) kwa ajili ya waamuzi wa madaraja ya Tatu na Pili ili kuweza kuwapandisha madaraja kwa mujibu wa utaratibu.
October 09, 2017
Read More
RWANDA na Sudani zimethibitisha kushiriki katika mashindano ya kuogelea ya kanda ya tatu ya Afrika (Cana zone 3) yaliyopangwa kufanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba 19 -21.
September 26, 2017
Read More
HABARI ZA JUU
KITAIFA
SERIKALI haitaweza kuwavumilia watendaji wazembe katika suala zima la uvamizi wa mifugo hususan ng’ombe kutoka katika nchi jirani ya Kenya.
October 16, 2017
Read More
NAIBU Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa ameishauri Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Kilimo ukanda wa Kitropiki (IITA) kuongeza kasi ya utoaji elimu kwa wakulima nchini kuhusu kadhia ya Sumu Kuvu.
October 16, 2017
Read More
WANACHAMA wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) 113 kutoka bara na visiwani wamejitokeza kuwania nafasi ya uenyekiti Taifa katika uchaguzi utakaofanyika mwaka huu, idadi ambayo haijawahi kutokea tangu kuanzishwa kwa umoja huo.
October 16, 2017
Read More
HATIMAYE Katibu Mkuu wa Baraza la Mashirika ya Kiislamu Nchini, Sheikh ISSA PONDA, leo amejisalimisha katika Kituo cha Polisi cha Central, kufuatia agizo la Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam, LAZARO MAMBOSASA.
October 13, 2017
Read More