UHURU FM
Panama yatangaza siku kuu baada ya kufuzu kwa Kombe la Dunia

RAIS wa Panama ametangaza siku ya Jumatano kuwa siku ya mapumziko baada ya nchi hiyo kufuzu michuano ya Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza.

Rais Juan Carlos Varela‏ aliandika ujumbe kwenye ukurasa wa mtandao wa kijamii wa twitter akidai kuwa sauti za watu zimesikika hivyo Jumatano ni siku ya mapumziko kitaifa

Panama iliifunga Costa Rica mabao 2-1 mjini Panama City jana.

Rais amesema kuwa wafanyakazi wa umma na wale wa makampuni ya kibinafsi watapumzika na pia shule hazitafunguliwa.

Watu nchini Panama walisherekea usiku kucha baada ya ushindi huo.

Hata hivyo kumekuwa na utata ikiwa goli la kwanza la Panama lilivuka mstari wa goli. 

RECENTS
MICHEZO
KOCHA wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars Salum Mayanga ameita kikosi cha wacheza 24 watakaoingia kambini kwa ajili ya mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Benin.
October 24, 2017
Read More
Mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya Young Africans na Simba utafanyika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam kama ilivyotangazwa awali. Hakuna mabadiliko.
October 23, 2017
Read More
HABARI ZA JUU
KITAIFA
BUNGE limepitisha marekebisho ya sheria ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya wa mwaka 2017 yenye lengo la kuboresha utekelezaji wa sheria na kuondoa upungufu uliojitokeza wakati wa kuitumia sheria hiyo.
November 17, 2017
Read More
MAAFISA kutoka Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Abeid Amani Karume cha Zanzibar (AAKIA), wamefurahishwa na namna ulinzi na usalama wa abiria na mali zao unavyofanywa kwenye Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), imeelezwa.
November 15, 2017
Read More
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan leo amefungua mkutano wa pili wa Biashara, Ujasiriamali na Maonyesho wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ulioandaliwa na Baraza la Biashara la Afrika Mashariki.
November 14, 2017
Read More
KATIKA kuhakikisha Vijana wengi zaidi wanapata Elimu ya Ufundi, Serikali inaendelea na Mpango wake wa Ujenzi wa Vyuo vya Ufundi 43 katika Wilaya mbalimbali nchini.
November 14, 2017
Read More