UHURU FM
Mama Maria Nyerere awataka watanzania kushikamana

Katika kuadhimisha Kumbukumbu ya miaka 18 ya Kifo cha Baba wa Taifa, Mjane wa Baba wa Taifa, Mama MARIA NYERERE, amesema wananchi wanatakiwa kushikamana ili kuleta maendeleo nchini.

Mama MARIA amesema Nyumbani kwake Mikocheni wakati Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kinondoni ilipokwenda kufanya usafi wa mazingira eneo hilo ikiwa ni sehemu ya Kumuenzi Muasisi wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.

Kamati hiyo iliyoongozwa na Mwenyekiti wake, ALLY HAPI, ilifika Nyumbani kwa Mama Maria ikiwa na Askari 417 kutoka idara mbalimbali likiwamo Jeshi la Wananchi wa Tanzania-JWTZ, Jeshi la Kujenga Taifa-JKT, Magereza pamoja na Jeshi la Polisi.

HAPI ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni kupitia kufanya Usafi wa Makazi hayo ni njia mojawapo ya kumuenzi Baba wa Taifa kwa vitendo.

Mwalimu NYERERE alipingana na maadui Watatu ambao ni Ujinga, Maradhi na Umasikini hivyo usafi ni sehemu ya kuunga mkono vita aliyoianzisha hasa kupinga maradhi yanayotokana na uchafu ya mazingira.

Kumbukumbu ya Baba wa Taifa inafanyika nchini kesho.  

RECENTS
MICHEZO
KUTAKUWA na mtihani na zoezi la utimamu wa mwili (Fitness Test) kwa ajili ya waamuzi wa madaraja ya Tatu na Pili ili kuweza kuwapandisha madaraja kwa mujibu wa utaratibu.
October 09, 2017
Read More
RWANDA na Sudani zimethibitisha kushiriki katika mashindano ya kuogelea ya kanda ya tatu ya Afrika (Cana zone 3) yaliyopangwa kufanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba 19 -21.
September 26, 2017
Read More
HABARI ZA JUU
KITAIFA
SERIKALI haitaweza kuwavumilia watendaji wazembe katika suala zima la uvamizi wa mifugo hususan ng’ombe kutoka katika nchi jirani ya Kenya.
October 16, 2017
Read More
NAIBU Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa ameishauri Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Kilimo ukanda wa Kitropiki (IITA) kuongeza kasi ya utoaji elimu kwa wakulima nchini kuhusu kadhia ya Sumu Kuvu.
October 16, 2017
Read More
WANACHAMA wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) 113 kutoka bara na visiwani wamejitokeza kuwania nafasi ya uenyekiti Taifa katika uchaguzi utakaofanyika mwaka huu, idadi ambayo haijawahi kutokea tangu kuanzishwa kwa umoja huo.
October 16, 2017
Read More
HATIMAYE Katibu Mkuu wa Baraza la Mashirika ya Kiislamu Nchini, Sheikh ISSA PONDA, leo amejisalimisha katika Kituo cha Polisi cha Central, kufuatia agizo la Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam, LAZARO MAMBOSASA.
October 13, 2017
Read More