UHURU FM
Polisi watoa angalizo kwa ma-admin wa makundi ya Whatsapp

JESHI la Polisi Kitengo cha Makosa ya Mtandaoni, limewatahadharisha viongozi wa Makundi ya What's App na kuwataka kutoa taarifa pindi uhalifu unapofanyika kwenye Makundi yao.

Kufanya hivyo kutasaidia Polisi kuchukua hatua dhidi ya mhusika aliyefanya uhalifu huo ili kukabiliana na ongezeko la vitendo vya uhalifu Mtandaoni.

Wito huo umetolewa leo na Naibu Mkuu wa Kitendo hicho, JOSHUA MWANGASA wakati wa semina iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Nchini-TCRA na kuwakutanisha viongozi wa Dini wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Amesema makosa ya Kimtandao yameendelea kuongezeka kwa kasi kubwa huku makundi ya What's App yakionekana kuwa kichocheo kikubwa, hivyo Makundi hayo hawatakiwi kuvumilia makosa hayo na badala yake wanatakiwa watoe taarifa Polisi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, JAMES KILABA, amesema Simu za Mkononi kwa sasa zimekuwa kama Silaha hivyo matumizi yake yanatakiwa kuangaliwa kwa umakini zaidi.

RECENTS
MICHEZO
KUTAKUWA na mtihani na zoezi la utimamu wa mwili (Fitness Test) kwa ajili ya waamuzi wa madaraja ya Tatu na Pili ili kuweza kuwapandisha madaraja kwa mujibu wa utaratibu.
October 09, 2017
Read More
RWANDA na Sudani zimethibitisha kushiriki katika mashindano ya kuogelea ya kanda ya tatu ya Afrika (Cana zone 3) yaliyopangwa kufanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba 19 -21.
September 26, 2017
Read More
HABARI ZA JUU
KITAIFA
SERIKALI haitaweza kuwavumilia watendaji wazembe katika suala zima la uvamizi wa mifugo hususan ng’ombe kutoka katika nchi jirani ya Kenya.
October 16, 2017
Read More
NAIBU Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa ameishauri Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Kilimo ukanda wa Kitropiki (IITA) kuongeza kasi ya utoaji elimu kwa wakulima nchini kuhusu kadhia ya Sumu Kuvu.
October 16, 2017
Read More
WANACHAMA wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) 113 kutoka bara na visiwani wamejitokeza kuwania nafasi ya uenyekiti Taifa katika uchaguzi utakaofanyika mwaka huu, idadi ambayo haijawahi kutokea tangu kuanzishwa kwa umoja huo.
October 16, 2017
Read More
HATIMAYE Katibu Mkuu wa Baraza la Mashirika ya Kiislamu Nchini, Sheikh ISSA PONDA, leo amejisalimisha katika Kituo cha Polisi cha Central, kufuatia agizo la Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam, LAZARO MAMBOSASA.
October 13, 2017
Read More