UHURU FM
Wizara ya Madini kufanya mnada wa Tanzanite

WIZARA ya Madini kwa mara ya Kwanza itafanya Mnada wa Madini ya Tanzanite kutoka katika Kampuni Nne za Uchimbaji na Biashara ya Madini katika eneo la Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Mnada ambao utafanyika Jumapili ijayo.

Kaimu Kamishna Msaidizi sehemu ya Uchumi na Biashara ya Madini, GODLEADER SHOO, amesema utaratibu wa kufanya Mnada wa Tanzanite ni jitihada za Serikali za kudhibiti utoroshwaji wa Madini nje nchi na pia kuwasaidia Wachimbaji kuuza Madini kwa bei ya ushindani inayoendana na Soko la Dunia.

Mnada huo utashirikisha wanunuzi kutoka ndani na nje ya nchi, ambapo atakayefanikiwa kununua Madini hayo ni yule tu atakayeshinda bei iliyowekwa kwa ajili ya kununua Madini husika.

Zoezi hilo linafanyika kwa njia ya uwazi kwa kushirikisha Wachimbaji, Wanunuzi, Shirika la Madini la Taifa-STAMICO, Vikosi vya Ulinzi na Usalama, Mamlaka ya Mapato Nchini-TRA, Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro na Wizara ya Madini.

RECENTS
MICHEZO
KUTAKUWA na mtihani na zoezi la utimamu wa mwili (Fitness Test) kwa ajili ya waamuzi wa madaraja ya Tatu na Pili ili kuweza kuwapandisha madaraja kwa mujibu wa utaratibu.
October 09, 2017
Read More
RWANDA na Sudani zimethibitisha kushiriki katika mashindano ya kuogelea ya kanda ya tatu ya Afrika (Cana zone 3) yaliyopangwa kufanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba 19 -21.
September 26, 2017
Read More
HABARI ZA JUU
KITAIFA
SERIKALI haitaweza kuwavumilia watendaji wazembe katika suala zima la uvamizi wa mifugo hususan ng’ombe kutoka katika nchi jirani ya Kenya.
October 16, 2017
Read More
NAIBU Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa ameishauri Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Kilimo ukanda wa Kitropiki (IITA) kuongeza kasi ya utoaji elimu kwa wakulima nchini kuhusu kadhia ya Sumu Kuvu.
October 16, 2017
Read More
WANACHAMA wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) 113 kutoka bara na visiwani wamejitokeza kuwania nafasi ya uenyekiti Taifa katika uchaguzi utakaofanyika mwaka huu, idadi ambayo haijawahi kutokea tangu kuanzishwa kwa umoja huo.
October 16, 2017
Read More
HATIMAYE Katibu Mkuu wa Baraza la Mashirika ya Kiislamu Nchini, Sheikh ISSA PONDA, leo amejisalimisha katika Kituo cha Polisi cha Central, kufuatia agizo la Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam, LAZARO MAMBOSASA.
October 13, 2017
Read More