UHURU FM
Kampeni ya Gusa Maisha Yao kufikia kilele chake kesho kwenye Viwanja vya Mwembeyanga

WAKATI kesho ikiwa ni hitimisho la Kampeni ya Uhuru Fm Gusa Maisha Yao, Awamu ya Kwanza, Meneja Utawala wa Kituo cha Uhuru FM, PAUL MNG`ONG`O, ametoa wito kwa Wakazi wa Mkoa wa Dar es salaam kujitokeza kwa wingi kesho katika Viwanja vya Mwembeyanga, Temeke, ili kushuhudia tamasha kubwa la Muziki.

Tamasha hilo ambalo linakwenda sambamba na kuadhimisha Kumbukumbu ya miaka 18 ya Kifo cha Baba wa Taifa, linatarajiwa kuanza Saa Tatu Asubuhi hadi Saa Kumi na Mbili Jioni.

Tamasha hilo ambalo halina kiingilio, ni hitimisho la Kampeni ya Uhuru FM ya Kampeni ya Gusa Maisha Yao ambayo ilianza kwa kutoa misaada mbalimbali kwa makundi yenye uhitaji katika Jamii.

RECENTS
MICHEZO
KUTAKUWA na mtihani na zoezi la utimamu wa mwili (Fitness Test) kwa ajili ya waamuzi wa madaraja ya Tatu na Pili ili kuweza kuwapandisha madaraja kwa mujibu wa utaratibu.
October 09, 2017
Read More
RWANDA na Sudani zimethibitisha kushiriki katika mashindano ya kuogelea ya kanda ya tatu ya Afrika (Cana zone 3) yaliyopangwa kufanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba 19 -21.
September 26, 2017
Read More
HABARI ZA JUU
KITAIFA
SERIKALI haitaweza kuwavumilia watendaji wazembe katika suala zima la uvamizi wa mifugo hususan ng’ombe kutoka katika nchi jirani ya Kenya.
October 16, 2017
Read More
NAIBU Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa ameishauri Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Kilimo ukanda wa Kitropiki (IITA) kuongeza kasi ya utoaji elimu kwa wakulima nchini kuhusu kadhia ya Sumu Kuvu.
October 16, 2017
Read More
WANACHAMA wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) 113 kutoka bara na visiwani wamejitokeza kuwania nafasi ya uenyekiti Taifa katika uchaguzi utakaofanyika mwaka huu, idadi ambayo haijawahi kutokea tangu kuanzishwa kwa umoja huo.
October 16, 2017
Read More
HATIMAYE Katibu Mkuu wa Baraza la Mashirika ya Kiislamu Nchini, Sheikh ISSA PONDA, leo amejisalimisha katika Kituo cha Polisi cha Central, kufuatia agizo la Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam, LAZARO MAMBOSASA.
October 13, 2017
Read More