UHURU FM
Mwakyembe aipongeza India kwa kuendelea kudumisha utamaduni wao

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dokta HARRISON MWAKYEMBE, ameipongeza India kwa kutimiza miaka 70 tangu ilipopata Uhuru kutoka kwa Uingereza mwaka 1947.

Waziri MWAKYEMBE, ametoa pongezi hizo Jijini Dar es Salaam wakati wa sherehe za maadhimisho hayo ambapo ameipongeza nchi hiyo kwa kuendelea kuuenzi na kuulinda Utamaduni wao hata wakiwa nje ya India.

Naye Balozi wa India hapa nchini, SANDEEP ARYA, ameishukuru Serikali kwa ushirikiano inaowapa katika maeneo mbalimbali yenye manufaa kwa Mataifa hayo mawili na kuahidi kuendeleza ushirikiano huo wa Kidiplomasia uliopo.

Katika sherehe hizo watu wa Jamhuri ya India walionyesha Utamaduni wao kwa kucheza Ngoma mbalimbali za Taifa hilo, Nyimbo, pamoja na Michezo mingine ya Kihindi ikiwa ni kuendeleza na kudumisha Utamaduni wa nchi hiyo.

RECENTS
MICHEZO
Leo Jumanne Januari 16, 2018 klabu ya Yanga imeingia mkataba wa miaka mitatu (3) na kampuni ya utengenezaji wa vifaa vya michezo ya Macron ambayo makao makuu yake yapo nchini Italy, Macron watakuwa ndio watengenezaji wakuu wa vifaa vyote michezo vya klabu hiyo.
January 16, 2018
Read More
Sekretarieti ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF imewapeleka kwenye kamati ya Maadili viongozi wanne kwa kughushi na udanganyifu.
January 16, 2018
Read More
HABARI ZA JUU
KITAIFA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 15 Februari, 2018 amemuapisha Luteni Jenerali Yacoub Hassan Mohamed kuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
February 15, 2018
Read More
Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini, imesema Mvua za Wastani Mpaka juu ya Wastani zinatarajiwa kuanza kunyesha katika kipindi cha wiki ya Kwanza ya Mwezi Machi hadi Mei mwaka huu katika maeneo mengi hapa nchini.
February 15, 2018
Read More
Serikali imesema imekamilisha uhakiki wa madai ya Watumishi wa Umma na kwamba kiasi cha shilingi Bilioni-43.39 ambacho ni madai halali kitalipwa kwa mkupuo pamoja na mshahara wa mwezi Februari mwaka huu.
February 09, 2018
Read More
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, imesema katika kipindi cha Mwezi Januari hadi Disemba mwaka jana, jumla ya Askari Polisi Mia Moja na Tano waliotenda makosa mbalimbali, walichukuliwa hatua za kinidhamu ikiwemo kufukuzwa kazi.
February 09, 2018
Read More