UHURU FM
TAMISEMI kupeleka Hati ya Drarura Bungeni kuhusu kufuta dhamana kwa atakayempa mimba mwanafunzi

SERIKALI kupitia Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa-TAMISEMI, imesema itapeleka Hati ya Dharula Bungeni ili itungwe sheria itakayofuta dhamana ya mtuhumiwa atakayempa ujauzito Mwanafunzi wa Shule ya Msingi na Sekondari.

Katika sheria hiyo uchunguzi wa Vinasaba-DNA utatakiwa kufanyika ili kuthibisha kama mtuhumiwa ndiye Baba wa Mtoto ama la.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa-TAMISEMI, JOSEPH KAKUNDA, ameelezea hatua hiyo Wilayani Mkalama Mkoani Singida, baada ya kutofurahishwa na taarifa kuhusu Wanafunzi 12 kukwamishwa masomo tangu mwezi Januari Mwaka huu kutokana na kupewa Ujauzito.

Kwa mujibu wa Naibu Waziri KAKUNDA, Wazazi wengi wamekuwa wakifanya makubaliano, ambapo Mwanafunzi aliyepewa ujauzito anamkana mhalifu aliyempa Ujauzito ili kumuepusha na kifungo cha miaka 30 Jela, jambo linalofanya kesi nyingi kukosa ushahidi.

RECENTS
MICHEZO
Leo Jumanne Januari 16, 2018 klabu ya Yanga imeingia mkataba wa miaka mitatu (3) na kampuni ya utengenezaji wa vifaa vya michezo ya Macron ambayo makao makuu yake yapo nchini Italy, Macron watakuwa ndio watengenezaji wakuu wa vifaa vyote michezo vya klabu hiyo.
January 16, 2018
Read More
Sekretarieti ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF imewapeleka kwenye kamati ya Maadili viongozi wanne kwa kughushi na udanganyifu.
January 16, 2018
Read More
HABARI ZA JUU
KITAIFA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 15 Februari, 2018 amemuapisha Luteni Jenerali Yacoub Hassan Mohamed kuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
February 15, 2018
Read More
Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini, imesema Mvua za Wastani Mpaka juu ya Wastani zinatarajiwa kuanza kunyesha katika kipindi cha wiki ya Kwanza ya Mwezi Machi hadi Mei mwaka huu katika maeneo mengi hapa nchini.
February 15, 2018
Read More
Serikali imesema imekamilisha uhakiki wa madai ya Watumishi wa Umma na kwamba kiasi cha shilingi Bilioni-43.39 ambacho ni madai halali kitalipwa kwa mkupuo pamoja na mshahara wa mwezi Februari mwaka huu.
February 09, 2018
Read More
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, imesema katika kipindi cha Mwezi Januari hadi Disemba mwaka jana, jumla ya Askari Polisi Mia Moja na Tano waliotenda makosa mbalimbali, walichukuliwa hatua za kinidhamu ikiwemo kufukuzwa kazi.
February 09, 2018
Read More