UHURU FM
Almasi iliyopatikana nchini Sierra Leone kuuzwa mjini New York

ALMASI ya karati 709 ambayo iligunduliwa na kundi la wachimba migodi nchini Sierra Leone mapema mwaka huu imeuzwa kwenye mnada hii leo mjini New York.

Ni almasi ya 14 kwa ukubwa kuwai kupatikana duniani na pia ndiyo kubwa zaidi kuwai kupatikana nchini Sierra Leon tangu mwaka 1972.

Jiwe hilo la thamani liligunduliwa na Emmanuel Momoh, mhubiri wa kikiristo kwenye wilaya iliyo mashariki ya Kono

Aliamua kuiuzua kwa serikali badala ya kuwauzia madalali.

Bw. Momoh aliiambaia BBC kuwa kwa kuiuza almasi hiyo kwa madalali hakungeinufaisha jamii.

Kuuzwa kwa almasi hiyo hiyo kunafanywa na kampuni inalojulikana kama Rapaport.

Mwenyekiti wa kampuni hiyo Martin Rapaport aliiambia BBC kuwa almasi hiyo ni ya kupendeza..

Alisema kuwa kutoka kutoka kwa almasi hiyo zinaenda nchini Sierra Leone na kwamba fedha hizo zitasaidia jamii ambapo ilipatikana.

Source: BBC

RECENTS
MICHEZO
Leo Jumanne Januari 16, 2018 klabu ya Yanga imeingia mkataba wa miaka mitatu (3) na kampuni ya utengenezaji wa vifaa vya michezo ya Macron ambayo makao makuu yake yapo nchini Italy, Macron watakuwa ndio watengenezaji wakuu wa vifaa vyote michezo vya klabu hiyo.
January 16, 2018
Read More
Sekretarieti ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF imewapeleka kwenye kamati ya Maadili viongozi wanne kwa kughushi na udanganyifu.
January 16, 2018
Read More
HABARI ZA JUU
KITAIFA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 15 Februari, 2018 amemuapisha Luteni Jenerali Yacoub Hassan Mohamed kuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
February 15, 2018
Read More
Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini, imesema Mvua za Wastani Mpaka juu ya Wastani zinatarajiwa kuanza kunyesha katika kipindi cha wiki ya Kwanza ya Mwezi Machi hadi Mei mwaka huu katika maeneo mengi hapa nchini.
February 15, 2018
Read More
Serikali imesema imekamilisha uhakiki wa madai ya Watumishi wa Umma na kwamba kiasi cha shilingi Bilioni-43.39 ambacho ni madai halali kitalipwa kwa mkupuo pamoja na mshahara wa mwezi Februari mwaka huu.
February 09, 2018
Read More
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, imesema katika kipindi cha Mwezi Januari hadi Disemba mwaka jana, jumla ya Askari Polisi Mia Moja na Tano waliotenda makosa mbalimbali, walichukuliwa hatua za kinidhamu ikiwemo kufukuzwa kazi.
February 09, 2018
Read More