UHURU FM
Wachimbaji wadogo wa madini watakiwa kujiunga kwenye vikundi

WACHIMBAJI Wadogo wa Madini Nchini wamesisitizwa kujiunga kwenye vikundi ili iwe rahisi kusaidiwa. Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo ametoa wito huo hivi karibuni Wilayani Ruangwa Mkoani Lindi, kwenye mkutano wake na Wachimbaji Wadogo wa Madini

ya Dhahabu na Vito (Green Garnet) wa Namungo wilayani humo.

Nyongo alisema dhamira ya Serikali ni kuwasaidia wachimbaji wadogo kuwa na uchimbaji wenye manufaa kwao na Taifa kwa ujumla na ili kufikia dhamira hiyo ni vyema wakajiunga kwenye vikundi.

"Mkijiunga kwenye vikundi itakua ni rahisi kuwafikia kwa pamoja na kuwapatia misaada mbalimbali yenye tija kwenye shughuli zenu," alisema.

Alisisitiza kwamba umoja ni nguvu, na ili mchimbaji awe na uwezo na nguvu kwenye utekelezaji wa majukumu yake inabidi afanye kazi akiwa ndani ya umoja na wenzake.

Alisema pale ambapo wachimbaji watakua wamejiunga kwenye vikundi, itakua rahisi hata kwa Taasisi za kifedha kuweza kuwafikia na kuwasaidia ikiwemo kuwapatia elimu ya fedha na vilevile mikopo.

"Nimekuja hapa kuzungumza nanyi ili kubaini changamoto zinazowakabili kwa ajili ya kuzitafutia ufumbuzi, na pia ninawaasa mhakikishe mnajiunga kwenye vikundi," alisema.

Aliongeza kwamba Serikali ingependa kuona Wachimbaji Wadogo wa Madini wanafanikiwa kufikia kwenye uchimbaji wa Kati na baadaye kuwa Wachimbaji Wakubwa.

Aidha, Wachimbaji hao walimuomba Naibu Waziri Nyongo kuendelea kuwatembelea mara kwa mara ili kuelewa changamoto zinazowakabili na kuzifanyia kazi kila inapobidi.

Baada ya kuzungumza na wachimbaji hao, Naibu Waziri Nyongo alitembelea Mgodi wa Dhahabu unaomilikiwa na Kampuni ya Germin Exploration ya Namungo huko Ruangwa na kukagua shughuli zinazofanywa na mgodi huo.

Vilevile alitembelea mradi wa kuchimba Madini ya Kinywe (Graphite) wa Kampuni ya PACCO GEMS LTD iliyopo katika vijiji vya Mtondo na Nanjaru wilayani humo ambapo aliahidi kuwasaidia kumaliza tatizo la upatikanaji wa hati ya umiliki wa ardhi wanayohitaji ili mradi uweze kuanza mara moja.

 

 

RECENTS
MICHEZO
Leo Jumanne Januari 16, 2018 klabu ya Yanga imeingia mkataba wa miaka mitatu (3) na kampuni ya utengenezaji wa vifaa vya michezo ya Macron ambayo makao makuu yake yapo nchini Italy, Macron watakuwa ndio watengenezaji wakuu wa vifaa vyote michezo vya klabu hiyo.
January 16, 2018
Read More
Sekretarieti ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF imewapeleka kwenye kamati ya Maadili viongozi wanne kwa kughushi na udanganyifu.
January 16, 2018
Read More
HABARI ZA JUU
KITAIFA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 15 Februari, 2018 amemuapisha Luteni Jenerali Yacoub Hassan Mohamed kuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
February 15, 2018
Read More
Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini, imesema Mvua za Wastani Mpaka juu ya Wastani zinatarajiwa kuanza kunyesha katika kipindi cha wiki ya Kwanza ya Mwezi Machi hadi Mei mwaka huu katika maeneo mengi hapa nchini.
February 15, 2018
Read More
Serikali imesema imekamilisha uhakiki wa madai ya Watumishi wa Umma na kwamba kiasi cha shilingi Bilioni-43.39 ambacho ni madai halali kitalipwa kwa mkupuo pamoja na mshahara wa mwezi Februari mwaka huu.
February 09, 2018
Read More
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, imesema katika kipindi cha Mwezi Januari hadi Disemba mwaka jana, jumla ya Askari Polisi Mia Moja na Tano waliotenda makosa mbalimbali, walichukuliwa hatua za kinidhamu ikiwemo kufukuzwa kazi.
February 09, 2018
Read More