UHURU FM
Kiongozi mwingine akiapishwa litakuwa kosa la uhaini Kenya

MWANASHERIA mkuu wa Kenya Prof Githu Muigai amesema jaribio lolote la kumuapisha kiongozi mwingine wa Kenya litakuwa ni uhaini wa hali ya juu.

Prof Muigai amesema hayo huku kiongozi wa upinzani nchini humo Raila Odinga akisisitiza kwamba ataapishwa kuwa rais Jumanne wiki ijayo.

Bw Odinga alitangaza mwezi uliopita kwamba ataapishwa na Mabunge ya Wananchi ambayo yalipendekezwa na muungano wa upinzani National Super Alliance (Nasa).

Ingawa hakumtaja mtu yeyote, Prof Muigai, akiwahutubia wanahabari Nairobi, alisema shughuli hama hiyo ya kumuapisha kiongozi ambaye hajatangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (IEBC) haina msingi wowote kikatiba na kwamba itakuwa "bure na batili".

"Sheria za jinai za Jamhuri ya Kenya zinazungumzia shughuli kama hiyo kuwa uhaini wa hali ya juu," amesema.

"Wanaoshiriki watakuwa wanajihusisha katika uhaini wa hali ya juu, pamoja na wote wanaofanikisha shughuli kama hiyo."

Adhabu ya kosa la uhaini kwa mujibu wa sheria za Kenya ni kifo.

Prof Muigai amesema Mabunge ya Wananchi ambayo yanaundwa na Nasa pia ni kinyume cha sheria.

Kufikia sasa, mabunge 12 ya majimbo, ikiwa ni pamoja na Mombasa, ambayo yanaongozwa na magavana wa muungano wa Nasa tayari yamepitisha azimio la kuundwa kwa mabunge hayo ya wananchi.

Kenya kwa jumla ina majimbo 47.

Nasa ilipendekeza kuundwa kwa mabunge hayo kama njia ya kushinikiza mageuzi nchini humo baada ya kususia uchaguzi wa marudio uliofanyika tarehe 26 Oktoba.

Rais Uhuru Kenyatta alitangazwa mshindi wa uchaguzi huo ambao ulisusiwa na upinzani.

Alipata kura 7.5 milioni, sawa na asilimia 98 ya kura zilizopigwa ingawa waliojitokeza walikuwa asilimia 39.

Bw Kenyatta aliapishwa kuwa rais tarehe 28 Novemba kwenye sherehe ambayo upinzani ulisusia.

Bw Odinga amesisitiza kwamba muungano wake hautambui ushindi wa Kenyatta na kwamba hautamtambua kama kiongozi halali wa nchi hiyo.

Marekani imemtaka Bw Odinga kuacha mpango huo wake wa kuapishwa kama rais wa nchi hiyo.

Waziri msaidizi wa Marekani kuhusu masuala ya Afrika, Donald Yamamoto ambaye alikuwa amezuru Kenya alimtahadharisha Bw Odinga na pia akahimiza kuwepo mashauriano kati yake na serikali iliyopo madarakani.

Aidha alitahadharisha dhidi ya matendo ambayo yako nje ya katiba nchini humo.

Source: BBC

RECENTS
December 07, 2017
MICHEZO
Kocha Mkuu wa Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’, Ammy Conrad Ninje amepanga kesho Jumanne Desemba 5, 2017 kuanza kufanyia kazi upungufu ulioonekana kwenye mchezo dhidi ya Libya uliofanyika Jumapili Desemba 3, mwaka huu.
December 04, 2017
Read More
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya Bakhresa Limited, Abubakar Bakhresa wameteuliwa kwenye Kamati za Maandalizi ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 (AFCON U-17) mwaka 2019 nchini.
December 04, 2017
Read More
HABARI ZA JUU
KITAIFA
TUME ya Taifa ya Uchaguzi-NEC, imevitaka Vyama vya Siasa kusoma na kuzingatia sheria zote za Uchaguzi kabla ya kuilalamikia na kuishnikiza kufanya maamuzi ambayo ni kinyume cha Sheria.
December 12, 2017
Read More
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi, Rais John Magufuli, ametangaza kuwa atafuta utaratibu wa sasa wa Idadi ya Wabunge kutoka Jumuiya za CCM na badala yake ataweka uwiano wa Nusu kwa Nusu kwa idadi ya Wabunge kutoka Jumuiya katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
December 12, 2017
Read More
MWANAJESHI wa zamani wa Mareknai ambaye alihamia Korea Kaskazini na kuwa mfungwa kwa karibu miaka 40 amefariki.
December 12, 2017
Read More
WAJUMBE wa Mkutano Mkuu wa Tisa wa Jumuiya ya Vijana ya Chama Cha Mapinduzi-UVCCM, wamemchagua kwa kishindo KHERI JAMES, kuwa Mwenyekiti Mpya wa Jumuiya hiyo, akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Sadifa Juma Khamis.
December 11, 2017
Read More