UHURU FM
CCM yawataka wanachama wake wenye sifa kujitokeza kuchukua fomu za ubunge na udiwani

CHAMA Cha Mapinduzi kimewatangazia Wanachama wake wenye sifa kujitokeza katika Ofisi za Wilaya za Chama hicho kuchukua Fomu za kuomba kuteuliwa kugombea Ubunge katika uchaguzi wa marudio katika Majimbo ya Singida Kaskazini, Longido na Songea Mjini.

Pia kutakuwa na Uchaguzi wa marudio wa Madiwani katika Kata Sita.

Wakati Chama Cha Mapinduzi kikitangaza utaratibu huo, habari kutoka ndani ya Chama Cha Democrasia na Maendeleo-CHADEMA kupitia kikao chake cha Kamati Kuu kinachoendelea, inadaiwa kuwa kitatangaza Chama hicho kujitoa rasmi katika kushiriki uchaguzi huo wa marudio.

Kwa mujibu wa Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa CCM, HUMPHREY POLEPOLE, fomu kwa ajili ya kuomba kuteuliwa kugombea Ubunge katika uchaguzi mdogo zimeshanza kutolewa tangu Disemba 5 hadi Disemba 9 mwaka huu, ambapo vikao husika vitakaa kwa ajili ya uamuzi wa mwisho.

Kwa mujibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi-NEC, uchaguzi wa marudio katika Majimbo Matatu na Kata Sita utafanyika Januari mwakani.        

RECENTS
December 07, 2017
MICHEZO
Kocha Mkuu wa Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’, Ammy Conrad Ninje amepanga kesho Jumanne Desemba 5, 2017 kuanza kufanyia kazi upungufu ulioonekana kwenye mchezo dhidi ya Libya uliofanyika Jumapili Desemba 3, mwaka huu.
December 04, 2017
Read More
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya Bakhresa Limited, Abubakar Bakhresa wameteuliwa kwenye Kamati za Maandalizi ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 (AFCON U-17) mwaka 2019 nchini.
December 04, 2017
Read More
HABARI ZA JUU
KITAIFA
TUME ya Taifa ya Uchaguzi-NEC, imevitaka Vyama vya Siasa kusoma na kuzingatia sheria zote za Uchaguzi kabla ya kuilalamikia na kuishnikiza kufanya maamuzi ambayo ni kinyume cha Sheria.
December 12, 2017
Read More
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi, Rais John Magufuli, ametangaza kuwa atafuta utaratibu wa sasa wa Idadi ya Wabunge kutoka Jumuiya za CCM na badala yake ataweka uwiano wa Nusu kwa Nusu kwa idadi ya Wabunge kutoka Jumuiya katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
December 12, 2017
Read More
MWANAJESHI wa zamani wa Mareknai ambaye alihamia Korea Kaskazini na kuwa mfungwa kwa karibu miaka 40 amefariki.
December 12, 2017
Read More
WAJUMBE wa Mkutano Mkuu wa Tisa wa Jumuiya ya Vijana ya Chama Cha Mapinduzi-UVCCM, wamemchagua kwa kishindo KHERI JAMES, kuwa Mwenyekiti Mpya wa Jumuiya hiyo, akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Sadifa Juma Khamis.
December 11, 2017
Read More