UHURU FM
Waziri Mkuu afungua jengo la Umoja wa Mataifa
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP. nchini, eneo la Mlimwa mjini Dodoma Desemba 7, 2017. Wapili kulia ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa UNDP Bw. Alvaro Rodriguez na wanne kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Dr. Augustine Mahiga.

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amezindua ofisi ya Umoja wa Mataifa na kusema uamuzi huo ni hatua muhimu ya kuendeleza mchakato wa Serikali wa kuhamia Dodoma. Ametoa kauli hiyo leo mchana (Alhamsi, Desemba 7, 2017) wakati akizungumza na viongozi na watumishi wa taasisi za Umoja wa Mataifa waliohudhuria hafla ya ufunguzi rasmi wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa Dodoma, katika eneo la Mlimwa, Manispaa ya Dodoma.

“Wote mtakubaliana nami kwamba uzinduzi wa ofisi hii ya Umoja wa Mataifa ni hatua muhimu sana ya kuendeleza mchakato wa Serikali wa kuhamia Dodoma. Pia, inafungua mlango mpya utakaowezesha ofisi zote za kibalozi na mashirika ya kimataifa kujenga ofisi zao hapa Dodoma na kuhamia mapema,” alisema.

Alisema anatambua kwamba kwamba wapo viongozi na watendaji wenye hofu ya kuhamia na kuanza maisha mapya Dodoma. “Baadhi ya watendaji wanaogopa changamoto za kuhamisha watoto wao na wenza wao ili kuanza maisha mapya. Napenda kuwatoa hofu kwamba Dodoma ni mahali pazuri pa kuishi na kuna fursa nyingi,” alisema.  Alisema Serikali inaendelea kuboresha miundombinu iliyopo ya huduma za jamii na miundombinu ya barabara, maji, umeme na mawasiliano ili iwe bora zaidi. Alitumia fursa hiyo kuwasihi waombe maeneo ya ujenzi kwa ajili ya ofisi na makazi.

Aliushukuru Umoja wa Mataifa kwa kuiteua Tanzania kuwa miongoni mwa nchi zinazotekeleza mfumo mpya wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa kuungana na kutekeleza shughuli zake kwa pamoja kama familia moja ya Umoja wa Mataifa yaani “UN Delivering as One”.

Naye Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Dk. Augustine Mahiga alisema Umoja wa Mataifa unayo mashirika 50 na kwamba mashirika 23 kati ya hayo, yanafanya kazi zake hapa nchini. Alisema wizara yake kwa kushirikiana na Manispaa ya Dodoma, watahakikisha kuwa mashirika hayo yanapatiwa viwanja vya kutosha ili kujenga ofisi zao mapema iwezekanavyo.

Mapema, Mwakilishi Mkazi wa UNDP na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania; Bw. Alvaro Rodriguez alisema wamefurahi kupata fursa ya kuwa taasisi ya kwanza ya  kimataifa kuwa na Ofisi yake kwenye makao makuu ya nchi hapa Dodoma

“Tumefurahi kujumuika kwa pamoja hapa Dodoma, lakini tunaahidi kuwa na sisi tutahamia kwa awamu kama ambavyo Serikali imekuwa ikifanya. Hili litategemea upatikanaji wa viwanja na majengo kwa ajili ya ofisi, kwa hiyo wafanyakazi wetu nao watahamia taratibu,” alisema.

RECENTS
MICHEZO
Leo Jumanne Januari 16, 2018 klabu ya Yanga imeingia mkataba wa miaka mitatu (3) na kampuni ya utengenezaji wa vifaa vya michezo ya Macron ambayo makao makuu yake yapo nchini Italy, Macron watakuwa ndio watengenezaji wakuu wa vifaa vyote michezo vya klabu hiyo.
January 16, 2018
Read More
Sekretarieti ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF imewapeleka kwenye kamati ya Maadili viongozi wanne kwa kughushi na udanganyifu.
January 16, 2018
Read More
HABARI ZA JUU
KITAIFA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 15 Februari, 2018 amemuapisha Luteni Jenerali Yacoub Hassan Mohamed kuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
February 15, 2018
Read More
Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini, imesema Mvua za Wastani Mpaka juu ya Wastani zinatarajiwa kuanza kunyesha katika kipindi cha wiki ya Kwanza ya Mwezi Machi hadi Mei mwaka huu katika maeneo mengi hapa nchini.
February 15, 2018
Read More
Serikali imesema imekamilisha uhakiki wa madai ya Watumishi wa Umma na kwamba kiasi cha shilingi Bilioni-43.39 ambacho ni madai halali kitalipwa kwa mkupuo pamoja na mshahara wa mwezi Februari mwaka huu.
February 09, 2018
Read More
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, imesema katika kipindi cha Mwezi Januari hadi Disemba mwaka jana, jumla ya Askari Polisi Mia Moja na Tano waliotenda makosa mbalimbali, walichukuliwa hatua za kinidhamu ikiwemo kufukuzwa kazi.
February 09, 2018
Read More