UHURU FM
Hatua TFF ilizochukuwa kwa mechi za ligi daraja la kwanza zenye malalamiko

Kwanza Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)  linapenda kumpongeza Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dr.Harrison Mwakyembe kwa ufuatiliaji wake wa karibu wa michezo ikiwemo Mpira wa Miguu. 

Baada ya mechi za Ligi Daraja la Kwanza (FDL)  Dodoma FC vs Alliance na Biashara vs Pamba kuliibuka malalamiko mengi ambayo yaliwafikia viongozi wakuu wa TFF na kuyatolea tamko. 

RAIS wa TFF Ndugu Wallace Karia alimuagiza Kaimu Katibu Mkuu wa TFF Ndugu Kidao Wilfred kufuatilia kwa kina jambo hilo ambapo hatua alizochukuwa Kaimu Katibu Mkuu ni pamoja na kuwasiliana na Kamishna wa mchezo na msimamizi wa Kituo cha Dodoma ambao wote walimpatia maelezo ya kilichotokea na baada ya hapo Kaimu Katibu Mkuu akawasiliana na Afisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi chombo kilichopewa dhamana ya kusimamia Ligi zote kubwa nchini ikiwemo Ligi Daraja la Kwanza, Afisa Mtendaji Mkuu naye alieleza Taarifa aliyopewa na Afisa wa Bodi aliyekuwa Dodoma. 

Kaimu Katibu Mkuu baada ya kuwasiliana na Afisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi alikuwa na mawasiliano yaliyochukuwa muda mrefu na Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo Ndugu Mohamed Kiganja ili kupata taarifa kutoka vyanzo mbalimbali kujiridhisha na jambo lililojitokeza.

Aidha Kaimu Katibu Mkuu amekuwa na mawasiliano na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo nchini Yusuph Singo kuhusiana na suala hilo mara baada ya michezo ile kumalizika na wamekuwa na ushirikiano mkubwa katika kulifuatilia jambo hilo kwa karibu.

Baada ya kupata taarifa mbalimbali Kaimu Katibu Mkuu alipeleka taarifa kwa Rais wa TFF ambaye aliagiza Kikao cha Kamati ya saa 72 kikae haraka iwezekanavyo ambapo Bodi ya Ligi walikuwa wanasubiri ripoti ambayo kwa mujibu wa kanuni za Ligi ni saa 48 na tayari taarifa zote zimefika jana kikao kimepangwa kufanyika kesho. 

Rais Karia bado aliona haitoshi hata kabla Waziri Mwakyembe "hajazungumza na Waandishi wa Habari" aliita Wana Habari na kati ya alivyozungumza ni kuhusu kinachoendelea Ligi Daraja la Kwanza na alionesha dhamira ya kuwashughulikia wote wanaotaka kuharibu Ligi zetu kwa Upana wake na kwa Ligi zote VPL, FDL na SDL na hasa kwa Michezo inayohusisha timu za Makundi yote zilizo katika nafasi ya kupanda au kushuka Daraja (FDL na SDL)  kuanzia mechi zinazolalamikiwa na kuhakiki za aina hiyo zisizolalamikiwa,lakini pia katoa maagizo kwa Kaimu Katibu Mkuu kuwaandikia barua TAKUKURU ili wachunguze matukio yote hayo yaliyojitokeza na yanayoendelea na TFF ipo tayari kutoa Ushirikiano wa kutosha katika Uchunguzi huo.

TFF inapenda kusisitiza kuwa viongozi wake wakuu hawajihusishi na jambo lolote lile la kupendelea mikoa wanayotoka ndiyo maana wakati Ndugu Wallace Karia alipokuwa Makamu wa Rais wa TFF timu tatu za Tanga Coast Union, African Sports na Mgambo zilishuka kwa mpigo. 

Katika mfumo wa kitaasisi unaoendesha TFF wenye jukumu la kusimamia Ligi zetu ni Bodi ya ligi, Ambao ndiyo wasimamizi wa moja kwa moja wa ligi daraja la kwanza hivyo maamuzi hufanywa kwa kutumia vyombo vya kitaasisi na hakuna nafasi kwa Rais wa TFF au Makamu wake kuingilia vyombo vya TFF ambavyo vinafanya kazi ya kusimamia ligi. 

TFF inawajibika kama msimamizi mkuu wa Soka nchini kuhakikisha vyombo vyake vinatenda haki kikiwemo chombo chake kinachosimamia ligi zetu TPLB. 

TFF pia kwa maelekezo ya Rais Karia kwa Kaimu Katibu Mkuu, ameelekeza kuangaliwa upya na Kufanyiwa marekebisho ya TIJA kwa Ratiba ya WAAMUZI (kama itabainika haja ya kufanya hivyo) kwa Michezo yote ya FDL inayokutanisha TIMU zenye nafasi ya kupanda au kushuka Daraja na Kuongeza USIMAMIZI katika Michezo hiyo. TFF itakuwa na Vikao vya Kiutendaji na BODI ya Ligi.

TFF pia inavitaka Vilabu na Wadau wake wote halali wanaotaka kurekodi Michezo ya FDL na SDL (ambayo hakuna TV iliyo na HAKI za kuonesha kwa sasa) kuwasiliana na TFF na Kupata KIBALI kitakacholinda HAKI zao na za Mchezo (TFF) kabla ya kufanya hivyo. Ni Makosa kurekodi mchezo wowote kwenye Mashindano ya TFF bila IDHINI ya TFF.

RECENTS
MICHEZO
Kimbembe cha Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL) kinaendelea leo Jumamosi (Januari 13, 2018) kwa mechi nane za raundi ya 13 kupigwa katika viwanja nane tofauti.
January 13, 2018
Read More
KOREA Kaskazini imesema kuwa itatuma ujumbe wake katika michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi 2018 inayotarajiwa kufanyika Korea Kusini mnamo mwezi Februari kulingana na mji wa Seoul.
January 09, 2018
Read More
HABARI ZA JUU
KITAIFA
NAIBU Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Dk.Abdulla Juma Saadalla ‘Mabodi’ amewasihi wananchi wa Tanzania kuendelea kuwaombea Dua na visomo mbali mbali Askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) wanaouawa wakilinda Amani katika nchini mbali mbali ikiwemo DRC Kongo.
January 22, 2018
Read More
WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amesema wizara yake haina mpango wa kuongeza tena muda zoezi la utambuzi wa mifugo na kuwataka wafugaji popote walipo nchini kupaza sauti zao ili kuhakikisha kuwa ng’ombe na punda wote wamepigwa chapa ifikapo Januari 31 mwaka huu.
January 20, 2018
Read More
ZOEZI la ugawaji wa Miguu ya kisasa ya bandia kwa watu wenye ulemavu wa Miguu awamu ya pili limeanza jana, ikiwa ni Kampeni iliyoanzishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda ya kuwapatia Miguu ya kisasa inayowawezesha kufanya shughuli za uzalishaji Mali Kama awali ambapo imejidhihirisha kuwa RC Makonda akiahidi jambo analitimiza kwa vitendo na sio Siasa.
January 20, 2018
Read More
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amewaagiza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasliano Prof. Makame Mbarawa Mnyaa na Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Zanzibar Balozi Ali Abeid Karume kusitisha usajili wa meli mpya hapa nchini mpaka hapo itakapotangazwa vinginevyo.
January 19, 2018
Read More