UHURU FM
Rais Dkt Magufuli aagana na Gavana wa BOT aliyemaliza muda wake Prof. Ndulu

RAIS Dkt John Pombe Magufuli, amemtaka Gavana Mteule wa Benki Kuu Profesa Florens Luoga, kufanya kazi ya kusimamia Uchumi wa Taifa kwa ufanisi mkubwa zaidi ili Nchi ipige hatua za Maendeleo kwa kasi zaidi.

Pia amempongeza Gavana anayemaliza muda wake Profesa BENNO NDULU kwa kumaliza huku hali ya Uchumi ikiwa nzuri, Taifa linakopesheka na kuna mazingira mazuri zaidi ya Uchumi kuendelea kukua.

Rais amesema hayo leo alipokua akiagana na Profesa NDULU Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Naye Gavana Mteule Profesa LUOGA amemshukuru Rais MAGUFULI kwa uteuzi huo na kumhakikishia ataisimamia BOT ili iendelee kuwa chombo imara cha kusimamia uchumi, kuisimamia fedha ya Tanzania na kuhakikisha nchi inatekeleza Miradi mikubwa ya Maendeleo.

Miradi hiyo ni Ujenzi wa Reli ya kati kwa kiwango cha kisasa, ujenzi wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere na Mradi wa umeme katika maporomoko ya Maji ya Mto Rufiji.

Baada ya mazungumzo yao Profesa NDULU amempongeza Rais kwa Miongozo muhimu iliyosaidia kuimarisha Uchumi ikiwemo kudhibiti mfumuko wa bei na kuongezeka kwa Akiba ya fedha za kigeni, hali ambayo imeimarisha uwezo wa Serikali kujiendesha na kugharamia Miradi mikubwa ya Maendeleo.

RECENTS
MICHEZO
Kimbembe cha Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL) kinaendelea leo Jumamosi (Januari 13, 2018) kwa mechi nane za raundi ya 13 kupigwa katika viwanja nane tofauti.
January 13, 2018
Read More
KOREA Kaskazini imesema kuwa itatuma ujumbe wake katika michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi 2018 inayotarajiwa kufanyika Korea Kusini mnamo mwezi Februari kulingana na mji wa Seoul.
January 09, 2018
Read More
HABARI ZA JUU
KITAIFA
NAIBU Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Dk.Abdulla Juma Saadalla ‘Mabodi’ amewasihi wananchi wa Tanzania kuendelea kuwaombea Dua na visomo mbali mbali Askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) wanaouawa wakilinda Amani katika nchini mbali mbali ikiwemo DRC Kongo.
January 22, 2018
Read More
WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amesema wizara yake haina mpango wa kuongeza tena muda zoezi la utambuzi wa mifugo na kuwataka wafugaji popote walipo nchini kupaza sauti zao ili kuhakikisha kuwa ng’ombe na punda wote wamepigwa chapa ifikapo Januari 31 mwaka huu.
January 20, 2018
Read More
ZOEZI la ugawaji wa Miguu ya kisasa ya bandia kwa watu wenye ulemavu wa Miguu awamu ya pili limeanza jana, ikiwa ni Kampeni iliyoanzishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda ya kuwapatia Miguu ya kisasa inayowawezesha kufanya shughuli za uzalishaji Mali Kama awali ambapo imejidhihirisha kuwa RC Makonda akiahidi jambo analitimiza kwa vitendo na sio Siasa.
January 20, 2018
Read More
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amewaagiza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasliano Prof. Makame Mbarawa Mnyaa na Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Zanzibar Balozi Ali Abeid Karume kusitisha usajili wa meli mpya hapa nchini mpaka hapo itakapotangazwa vinginevyo.
January 19, 2018
Read More